Skip to main content




UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI


Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.


Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.


Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:

1. Kuwa na kisa/wazo unalotaka kuliandikia

Katika jamii kuna mambo mengi sana yanayotendeka, msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo yanayotendeka katika jamii. Kama tujuavyo fasihi andishi kazi yake ni kuonesha yale yanayotendeka katika jamii, kwa hiyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo ili kuweka wazi mambo yanayoendelea katika jamii.


Kwa mfano mwandishi naweza kutunga kazi ya kibunifu kuhusu, ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha yake mwenyewe, ushirikina, jambo lolote analoliamini katika maisha (falsafa yake). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa msanii kabala ya kuandika ni kuelewa vizuri jambo analotaka kuandikia. Pia katika hatua hii msanii anaweza kubuni jina la hadithi yake, pia hii inaweza kumsaidia katika upangaji wa visa na matukio ya hadithi yake.

2. Kuchagua umbo la kazi ya fasihi

Msanii akishapata wazo la kuandika, sasa inambidi achague jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake hilo. Yaani anaweza kuchagua endapo aandike hadithi fupi, riwaya au tamthiliya, au ushairi au utenzi. Sasa uchaguzi wa umbo la kazi ya fasihi unategemeana na uwezo wa msanii katika tanzu hizo, kuna mwingine anapenda tamthiliya lakini kuandika riwaya hawezi, kuna mwingine anaona kuandika ushairi ni rahisi na kuna mwingine hawezi. Kwa hiyo ubunifu wa msanii utadhihirika katika utanzu ule anaoumudu vizuri zaidi.

3. Kubaini hadhira

Mwandishi kujua yule anayemwandikia ni suala la msingi sana. Hadhira ipo ya watu wa aina mbalimbali, watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa n.k. Sasa mwandishi akishabaini hadhira anayoindikia itamsaidia kuteua lugha ya kuandikia, kwa mfano kama ni watoto, hatutegemei mwandishi kutumia lugha ngumu, misemo na nahau nyingi.

4. Kubuni wahusika na mandhari

Mwandshi baada ya kujua kazi yake inahusu nini sasa inambidi abuni wahusika wa hadithi yake. Wahusika wanaweza kuwa ni watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika n.k. Pia ni lazima abaini mazingira ambamo visa vyote vya hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu n.k

5. Kupanga msuko wa visa na matukio

Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi. Sasa kama mwandishi amaeamua kuwasilisha kazi yake kwa njia ama ya hadithi fupi au riwaya au tamthiliya ni vema ajue namna visa na matukio vitakavyopangwa. Katika kufanya hivi maswali yafuatayo ni muongozo mzuri katika kupangilia ploti: Hadithi yangu itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Je, kilele cha mgogoro ni nini? Je, ni mhusika mkuu kubakwa na kuambukizwa VVU? Hadithi yangu inaishaje? Je mhusika mkuu ashindwe? Atorokee nje ya nchi? Afungwe? Abadilike Au maadui ndio wafungwe au wafe? Au wabadilike?

6. Kuanza kuandika

Sasa baada ya kupitia hatua hizo zote, mwandishi sasa anaweza kuanza kuandika. Mchakato wa kuandika hua ni mrefu na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika, hii ni kutokana na kwamba mambo mengi ya kuandika huwa yanakuja wakati mwandishi ameanza kuandika kazi husika. Hata hvyo sio vibaya kufanya hivi, hii pia inasaidi kuwa na zao bora la fasihi.







UTUNGAJI WA HADITHI


Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.


Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k


Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.




Mikondo ya Uandishi wa Hadithi


Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
1. Mkondo wa kiwasifu; mkondo huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
2. Mkondo wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
3. Mkondo wa kihistoria; hadithi katika mkondo huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
4. Mkondo wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
5. Mkondo wa kimapenzi; katika mkondo huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.


Utungaji wa Hadithi Fupi


Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
1. Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
2. Idadi ya wahusika ni ndogo ukilinganisha na wahusika wa kwenye riwaya.
3. Mandhari ya hadithi fupi si mapana kama ilivyo katika riwaya
4. Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi.




UTUNGAJI WA TAMTHILIYA


Tamthiliya ni kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lengo la kuonyeshwa jukwaani, ambapo wahusika huzungumza na kutenda vitendo mbalimbali. Tamthiliya huigiza maisha ya kila siku.
Kwa kuwa tamthiliya imeandikwa kwa lengo la kuigizwa huwa imeandikwa na maelezo ya jukwaani, maelezo yanayoonesha nini kifanywe na nani na kwa namna gani. Tamthilya hugawanywa katika maonyesho kama ambavyo riwaya inavyogawanywa katika sura.


Tamthiliya imegawanyika katika aina zifuatazo:
1. Tanzia; ni aina ya tamthiliya ambapo mhusika mkuu/shujaa anapata anguko kubwa au kifo ambacho huwafanya hadhira kuwa na huzuni.
2. Ramsa ni tamthilia ambayo hulenga kufundisha kwa njia ya kuchekesha ili kuleta ujumbe mzito.
3. Vichekesho/Futuhi ni aina ya tamthiliya ambayo lengo lake kuu ni kuchekesha kwa kutumia mbinu ya kutia chumvi mambo, kudhihaki na kukejeli.




Kutunga Tamthiliya


Katika utunzi wa tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, mambo hayo ni kama yafuatayo:
1. Chagua jambo unalotaka kuandikia
2. Panga namna msuko wa visa na matukioa utakavyokuwa
3. Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kukiandika
4. Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa vyako
5. Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika
6. Gawa tamthiliya katika maonyesho
7. Weka maelekezo ya jukwaa. Haya huelezea kile kinachotendeka kwa wakati ule. Maelezo ya jukwaa huwa katika maandishi ya italiki.

Popular posts from this blog

UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira. Au, Insha ya kisanaa ni ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali za semi. Muundo wa Insha Kwa kawaida insha inakuwa na sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi, kiini na hitimisho. a) Kichwa cha insha; Kichwa cha insha hudokeza kile utachokijadili katika insha yako, hubainisha wazo kuu la mada inayohusika. Kwa kawaida kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano; maisha ya kijijini, mimba za utotoni. b) Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangul...
Uhakiki wa Fani katika Ushairi Fani katika Ushairi wa Wasakatonge Hakiki fani katika Ushairi wa Wasakatonge MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS MWAKA: 2001 JINA LA KITABU Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa. MUUNDO Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano: Tathlitha: Haya ni mashairi ambayo ya...
MAENDELEO YA KISWAHILI ASILI YA KISWAHILI Neno asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Kutokana na fasili hii tunaona kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa. Hivyo basi asili ya lugha ya Kiswahili bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko la lugha ya kiswahili. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati na dini ya kiislamu. Wengine wanashikilia msimamo kuwa kiswahili ni kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na uchotara baadhi yao wanaoshikilia msimamo huu ni Freeman Grenville na Homo Sasson Kuna nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea asili ya Kiswahili, miongoni mwa hizo ni pamoja na hizi zifuatazo: Kiswahili ni Kiarabu Hapa Kiswahili kimefasiliwa kuwa asili yake ni kiarabu, wanaoshikilia mtazamo huu wanahoji kwamba katika lugha ya Kiswahili kuna maneno mengi ya Ki...
UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi. Maana ya Uhakiki Dhana ya Uhakiki Fafanua dhana ya uhakiki Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa kazi za kifaishi. AU kwa lugha rahisi tunaweza kusema, uhakiki ni uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi kama vile riwaya, tamthiliya na mashairi kwa lengo la kufafanua vipengele vya fani na maudhui. Misingi ya Uhakiki Elezea misingi ya uhakiki Kwa ujumla mhakiki wa kazi za fasihi anapofanya uhakiki wa kazi za kifasihi,...
MJENGO WA TUNGO Maana ya Tungo Tungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Au tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani ambayo huweza kuwa kamili au isiyo kamili. Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu tungo huanzia neno; rejea aina za tungo. AINA ZA TUNGO Tungo neno: Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano; anacheza, kakimbia. Tungo Kirai: ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu. Mfano; mtoto mzuri, kiyama chake, bondeni Tungo kishazi: Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe. KI...
NGELI ZA MANENO Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana. Mfano: 1. Maji yakimwagika hayazoleki 2. Mayai yaliyooza yananuka sana 3. Yai lililooza linanuka sana 4. Maji liliomwagika halizoleki Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi. Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi. Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo: 1. Hutumika kupanga majina ya lugha k...