
Uhakiki wa Fani katika Ushairi
Fani katika Ushairi wa Wasakatonge
Hakiki fani katika Ushairi wa Wasakatonge
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha: Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.Shairi la Ua.“Ua limejituliza mtini laning’inia,Mwenyewe laniliwaza, furahani lanitia, Ua sasa limepea, macho walikodolea.”
Tarbia: Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.Shairi la“Kifungo.” “Miaka imeshapita, sasa najiamkia,Naanza bila kusita, bahati kujitafutia,Hapo nitapoipata, mola jishukuria,Kifungo kimenichosha, minyororo nafungua.
Takhmisa: Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.Shairi la“Israfu”. “Mali ulojichumia,Ni yako nakubalia,Lakini kiangalia,Vipi unaitumia,Mwenzangu nakuusia israfu haifai.”
Sabilia: Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”.Shairi la“Punda”. “Toka ulipozaliwa, maishayo ni kizogo,Hujapata kuenziwa, waishi tiriigivyogo,Nawe hujajielewa, u kiumbe hu kigogo,Kama ungefadhiliwa, usingebeba mzigo, Hakika ulionewa, hustahili kipigo,Haki umeitambua, idadi japo kidogo.”
MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki” “Payuka

Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.
MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
Tamathali za Semi
Tashibiha: “Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” -Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
Tashihisi: “Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
Sitiari: “wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”
Mbinu nyingine za kisanaa
Onomatopea/ tanakali sauti: “kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
Takriri: “Charuka” – “charuka”
Tashititi: “Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”
Matumizi ya semi
Methali: “Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
Matumizi ya taswira
“Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”
“Ua” – mpenzi – “Ua”
“Punda”-wanyonge – “Punda”
“Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”
“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”
“Baharini” – nchi – “Sokomoko”
“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”

Fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
Hakiki fani katika Ushairi wa Mashairi ya Chekacheka
MWANDISHI: THEOBALD A. MVUNGI
WACHAPISHAJI: EDUCATIONAL PUBLISHERS AND DISTRIBUTORS LTD.
MWAKA: 1995
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa tarbia, mashairi yake yote yamefuata muundo huu. Beti za mashairi yake zina mistari minne. Mengi ya mashairi yake, mistari imegawanyika katika vipande viwili yaani mistari ina vina vya kati na vya mwisho. Mfano katika shairi la “Mashairi ya “Ngulu”;

Pia katika baadhi ya mashairi yake ameyaumba katika kipande kimoja, yaani yana kina cha mwisho tu. Mfano ni mashairi kama vile ya“Dhahabu ya fahari”, “Utu umekuwa kima”,“Seng’enge”mfano katika shairi la“Utu umekuwa kima”

MTINDO
Mtindo aliotumia mwandishi ni mtindo wa kimapokeo kwani amezingatia vigezo vya vina na mizani katika utunzi wa mashairi yake. Mfano katika shairi la”“Tuambae ukasuku”

MATUMIZI YA LUGHA
Tashibiha: “Mshairi jihadhari, usishikwe kama fimbo.” – “Tuambae ukasuku.”“Na wasiothaminiwa, wapimwao kama nyasi”- “Raia si mali kitu”“Mapenzi yasinadiwe, kama shati dukani” – “Penzi lisilo heshima”“Utaliwa kama pumba” – “Utaliwa kama pumba”“Kaburu si mtu hata, kwake sisi sawa punda” – “Utumwa huru”.“Pungufu akili yake, mla punje kama kuku” – “Tuambaeukasuku”
Tashihisi: “Mejaribu kujongea, ndege awe mkononi,Yeye juu hurukia, namuomba samahani.” – “Njiwa kiumbe mtini”“Moyo nimeshauri, lakini umekaidiMoyo kiburi hatari, mfanowe kama radiMoyo mefumbata shari, unayakwepa marudi,Moyo u mwilini mwangu, jirudi tuwe pamoja.” – “Moyo”Nipishe wewe senge’nge” – “Seng’enge”.“Kijiji kisichoringa” – “Mashairi ya Ngulu”.“Akili yamsaliti, kikongwe haoni kweli.”- “ Ni wapi ushauri?”
Sitiari: “Mshairi awe Nyati”- “Tuambae ukasuku”“Sisi ni miamba gogo”- “Raia si mali kitu”“Ile chai kikombeni, rangi yake Mwafrika” – “Chai”.“Kwetu ulikuwa mama” – “Indira”“Utu umekuwa kima” – “Utu umekuwa kima”“Uroho umekujaa, watu mefanya kondoo” – “Utaliwa kama pumba”
Matumizi ya semi
Misemo: “Fedha fedheha” – “Chanzo cha huo uozo”
Methali: “Akishaoza samaki, busara ni kumtupa” – “Chatu mmeza matonge”
Nahau: “Wabunge waote meno, wasivilambe viatu” –wawe na mamlaka– “Tuambae ukasuku”Mbinu nyingine za kisanaa
Takriri: “Chai ninaipa hati, kwa kutukidhia haja,Chai imewekwa kati, kwetu sisi sote waja,Chai majani ya miti, hii miti yenye tija.” – “Chai”Neno“njiwa” limejirudia katika kila ubeti –“Njiwa”Neno “moyo” limerudiwa katika kila ubeti. – “Moyo”Neno “mauti” limejirudia katika ubeti wa kwanza – “Utaliwakamapumba”Neno “Ngulu” katika mashairi ya “Ngulu”.
Ujenzi wa Taswira
“Matonge”- madaraka-“Mwinyi umewasha moto”“Nyati”– watawala –“Tuambae ukasuku”“Mfugaji”– mwananchi – “Tuambae ukasuku”“Jiko”– madaraka “Kuna nini huko jikoni”“Chatu”– watawala –“Chatu mmeza matonge”“Chura”– mtu asiye na msimamo - “Chura umegundulika”
Fani katika Ushairi wa Malenga Wapya
MWANDISHI: TAASISI YA KISWAHILI, ZANZIBAR
WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 2001
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande wa maudhui mambo yanayoelezwa mengi yanaigusa jamii ya sasa. Masuala ya maadili, siasa, uchumi, ukombozi wa kiutamaduni changamoto na suluhisho ya matatizo yanayoikumba jamii yanaendana na wakati wa sasa. Hivyo upya wa malenga wapya ni kweli. Kifani pia Malenga wapya wameweka muundo na mtindo wa kisasa.
MUUNDO
Tunapohakiki muundo katika ushairi tunaangalia idadi ya mistari katika ubeti. Ubeti huweza kuwa na mistari miwili, mitatu, minne na kuendelea. Aina za muundo zimepewa istilahi maalum kuutofautisha aina moja na nyingine mfano mashiri yenye mistari miwili katika ubeti ni Tathnia. Imetumika miundo tofautitofauti katika diwani hii. Mfano:
Tathlitha
Haya ni mashairi ambayo yana mistari mitatu kwa kila beti, mengi ya mashairi haya ni ya kisasa. Mfano ni shairi la“Hali halisi”, “Puuzo”, “Ua”, “Kuunge”, “Tunzo”.

Tarbia
Haya ni mashairi yenye mistari mine. Mfano ni shairi la“Kitendawili”, “Mkulima”, “Majonzi”, “Bahari”, “Samaki mtungoni” “Kifungo”,na mengine mengi.

Takhmisa
Haya huwa na muundo wa mistari mitano katika kila ubeti. Mfano ni mashairi ya“Siharakie maisha”, na “Israfu”.

Sabilia
Haya ni mashairi yenye mistari kuanzia sita na kuendelea. Mfano ni shairi la“Punda”na “Pasua uwape ukweli”

MTINDO
Imetumika mitindo ya aina zote mbili. Kwanza wametumia mtindo wa kisasa. Huu ni mtindo ambao haufuati kanuni za urari wa vina na mizani katika beti pia huitwa mashairi huru. Mtindo mwingine ni mtindo wa kimapokeo, huu hufuata kanuni na sheria zote za vina na mizani katika utunzi wake. Mara nyingi huwa na mistari minne katika kila ubeti.
Mfano wa mashairi yaliyotumia mtindo wa kisasa ni mashairi ya“Pasua uwape ukweli”, “Haki”. “Payuka”. Mfano shairi la Pasua uwape ukweli

Pia mfano wa mashairi ya kimapokeo ni shairi la“Mkulima”, “Bahari”, “Tuyazingatie haya” “Nipate wapi mwingine”.

MATUMIZI YA LUGHA
Diwani ya malenga wapya imetumia lugha yenye ubunifu bora wa kisanaa.Vilevile ni lugha rahisi na sanifu inayoeleweka kwa hadhira lengwa.
TAMATHALI ZA SEMI
Tashibiha: “Nizikwe kama wezangu, nisitupwe kama paka” -Shairi la“Nini wanangu”.“Hata pamoja muweko, ubaguzi umezama,kama nguzo” -Shairi la“Tunzo ubeti wa nne”.“Mfanowe kama radi, chini inapoanguka”.-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Nikabaki kama ng’onda” - Shairi la“Nipatieni dawa”.“Maisha ni kama njia”-Shairi la“Maisha ni kama njia”.“Yameotewa na kombe, mithili gome la mti”-Shairi la“Bahari ubeti wa pili”.
Tashihisi: “Ewe ulimi sikia” -Shairi la“Ulimi”.“Haki wa tutisha,tusikuandame,kwa matendo yetu” –Shairi la“Haki ubeti wa kwanza”.“Njiwa ameishanitoka, nipate wapi mwingine”-Shairi la“Nipate wapi mwingine”.“Samaki wasikitika, kudai walikotoka, Wote wamekasirika, uhuru wanachotaka,”-Shairi la“samaki mtungoni”.
Sitiari: “wamejipa uwezo wa Rabuka” – “Mpaka lini”“Paka shume jigeuza” – “Kwanini?”“mshumaa ” – “Hali halisi”Mbinu nyingine za kisanaa.
Onomatopea/ tanakali sauti: “kokoriko”- “Mkulima”“Parakacha” – “kwanini”.
Takriri: “Charuka” – “charuka”
Tashititi: “Nasikia mnatunga mwatungani washairi?” “mwabwaja mwasema nini”Matumizi ya semi
Methali: “Simwamshe asilani aliyelala usingizini” – “Payuka”“Fahali wapiganapo, nyasi ndio huumia”- “Sokomoko baharini”“Subira yavuta heri”- “Siharakie maisha”
Taswira: Matumizi ya taswira“Samaki” – wanyonge – “samaki mtungoni”“Ua” – mpenzi – “Ua”“Punda”-wanyonge – “Punda”“Mvuvi” – wanyonyaji – “Samaki mtungoni”“Njiwa” – mpenzi – “Nipate wapi mwingine”“Baharini” – nchi – “Sokomoko”;“Abiria”- wananchi –“Sokomoko”
Uhakiki wa Maudhui katika Kazi za Fasihi Andishi
Maudhui katika riwaya ya Takadini
Hakiki Maudhui katika riwaya ya Takadini
DHAMIRA
Dhamira kuu
Suala la imani potofu na ushirikina: Wanakijiji wa kijiji cha Sekai na wanakijiji wa kijiji cha Mtemi Makwati, wana imani potofu juu ya binadamu aliye na ulemavu wa ngozi yaani albino “sope” wanaamini kuwa kuzaliwa kwa mtoto wa aina hiyo ni laana na hapaswi kabisa kuishi. Hawaamini kuwa ni binadamu wa kawaida. Mfano uk.8Ambuya Shungu anasema“mtoto ni Musope.Ni wajibu wetu kumuharibu”.Mwandishi amelionesha suala hili makusudi ili jamii iweze kupinga na kuacha mila hizi potofu mara moja! Anaiasa jamii kuwapenda, kuwajali na kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi na si hivyo tu bali pia anaona upo umuhimu wa jamii kuwapa nafasi watu wa aina hiyo kwani wanaweza kuwa na umuhimu mkubwa na mchango katika jamii.
Dhamira ndogo ndogo
Ubaguzi kwa watu wenye ulemavu: Hii ni dhamira nyingine ambayo imejadiliwa ndani ya riwaya hii. Mwandishi anaonesha kuwa ubaguzi si mzuri kwani huwafanya watu wenye ulemavu wa ngozi wajisikie vibaya na kujiona si sehemu ya jamii wanayoishi. Tunaona jinsi Nhamoalivyombagua nakumtenga Takadini, uk. 62 “huwezi kukimbia na huwezi kupigana…..tena hata huoni vizuri. Ha! Wala hufanani hata na mmoja kati yetu, watu wanasema una laana, sitaki kuwa rafiki yako....anaendeleakumwambia“wewe ni sope, sope, sope!”kumbe tunapaswa kuwapenda na kuwajali watu wote bila ubaguzi.
Ndoa za mitara: Wanaume wa kijiji cha Sekai wana desturi ya kuoa mke zaidi ya mmoja. Mfano Makwati alikuwa na wake wanne ambao ni Sekai, Pindai, Dadirai na Rumbdzai. Wake hawa si wote walipendana bali walijitenga na kuoneana wivu mfano Dadirai na Rumbdzai hawakumpenda kabisa Sekai walimsimanga na kumsengenya. Mfano uk.15 Dadirai alisema kwa chuki “lazima atimuliwe hapa…. arudi kwao” “Ha! Atimuliwe tena? Ni mchawi!”hivyotunaona kuwa ndoa za mitara ni tatizo katika jamii kwani huweza kusababisha migogoro na ugomvi tena huweza kusababisha hata kuambukizana magonjwa hatari hasa katika kizazi cha leo ambapo magonjwa ni mengi ya hatari.
Mapenzi ya dhati na huruma: Mzee Chivero ni mzee aliyeonesha mapenzi ya dhati kwa Sekai na mwanae kwani aliwapokea na kuishi nao, pamoja na hali waliyokuwa nayo bila kuwabagua. Alimhurumia Takadini akampenda, kumsaidia na kumshauri vyema siku zote. Pia tunaona Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini kwani aliweza kumkinga na kumuokoa asiuawe. Mfano uk.10 Sekai anasema“hapana Ambuya mtoto lazima aishi. Hapana Ambuya mtoto ni wangu na sitamwachia mtu”…… sitamwachia mtu yeyote mwanangu”.
Nafasi ya mwanamke
Mwanamke amechorwa katika nafasi mbalimbali katika riwaya hii kukamilisha ujumbe wa mwandishi kwa jamii kuhusu wanawake.
Mwanamke amechorwa kama kiumbe jasiri: Sekai ameonekana kuwa na ujasiri wa hali ya juu kwani aliamua kupingana na mila za jamii yake na kuamua kutoroka na kitoto bila kujua alipoelekea ili tu kumuokoa mwanae. Hivo anapaswa kuigwa na jamii.
Amechorwa kama mwanamapinduzi: Sekai na Shingai wamechorwa kama wanawake wanamapinduzi kwa kuubadilisha mtazamo wa wanajamii wenzao kuhusu baadhi ya mila potofu. Mfano Shingai aliamua kuolewa na Takadini bila kujali ulemavu wake. Hakuogopa wazazi wake wala hakuogopwa kutengwa na ndipo badae jamii ilimkubali. Pia Sekai ni mwanamapinduzi kwa kuzikataa mila potofu ya kuwaua albino, alimtunza mwanae na kumlea mapaka akakua.
Amechorwa kama chombo cha starehe: Mwanamke katika jamii hizi alionekana kama chombo cha starehe tu kwani waliolewa wanawake wengi kwa mwanaume mmoja na lengo nikumburudisha tu na kumzalia watoto.
Amechorwa kama kiumbe dhaifu asiyeweza kusema chochote wala haki yoyote: Wazazi wa Shingai hawakumpa kabisa Shingai uhuru wa kuchagua mwanaume aliyempenda. Walimlazimisha kuolewa na mwanaume waliyemtaka. Mfano uk.118 Shingai anasema“huyu ndiye mtu ninayeteka anioe. Hakuna aliyeniuliza kama nampenda Nhamo. Wewe na baba mlikuwa na hamu ya kuniozesha katika familia ya Manyamombe hata matakwa yangu hayakusikilizwa. Sasa nimechagua”.
Amechorwa kama mtu mwenye mapenzi ya dhati: Sekai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanae Takadini. Pia Shingai alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na hata kuamua kuolewa naye.
Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mfano mzuri ni Sekai alivumilia kwa muda mrefu bila kukata tamaa kukosa uzazi, masimango ya wake wenzake na hatimaye alipata mtoto. Pia alivumilia kumlea Takadini wala hakuthubutu kumtenga hata mara moja bali alimvumilia mpaka alipokua.
MIGOGORO
Mgogoro kati ya Sekai na Rumbdzai na Dadirai: Sababu ya mgogoro huu ni kwamba, wanawake hawa wawili hawakumpenda kabisa Sekai na walimuonea wivu kwa kitendo cha kupendwa sana mumewe. Walimsimanga na kumsengenya muda mwingi na hasa kutokana na tatizo la Sekai la kukosa mtoto kwa muda mrefu. Walimwita mchawi.
Mgogoro kati ya Sekai na Makwati mumewe: Sababu ya mgogoro huu ni Sekai kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambapo katika jamii yao ni laana. Mumewe hakumwamini alimgombeza na kumtishia kumuua akidhani Sekai ni mchawi. Sekai na mwanae anaamua kutoroka ili kuondokana adha ile.
Mgogoro kati ya Nhamo na Takadini: Sababuni kuwa Nhamo alimpiga na kumdhalilisha Takadini mara kwa mara mbele ya vijana wengine kwakuwa ni Sope. Alimkejeli na kumdhihaki mfanouk.62 “wewe ni sope umelaaniwa”Nhamo alimwambia Takadini. Pia sababu nyingine ni kutokana na Shingai mchumba wa Nhamo kuwa na mapenzi ya dhati kwa Takadini na kumkataa yeye. Takadini alivumilia na kutolipiza kisasi na baadae alifanikiwa kumuoa Shingai na kuzaa naye mtoto wa kiume.
Mgogoro kati ya Nhariswa na mkewe: Nhariswa alimpiga na kumgombeza mkewe kwa kitendo cha kutomfuatilia binti yao na kumwacha aanzishe uhusiano na kijana aliyeaminiwa kuwa amelaaniwa.
Mgogoro kati ya Shingai na mama yake: Mgogoro huu ulitokana na Shingai kuamua kuolewa na Takadini jambo ambalo hawakulitaka kabisa kutokana na hali ya Takadini. Mama yake anaamua kumkana Shingai hadharani kuwa si mtoto wake tena.
Mgogoro kati ya Nhamo na Tapfumaneyi. Vijana hawa walipigana ili kumtafuta mshindi na shujaa bingwa wa mapigano. Vijana walipigana sawia na walitoka sawia.
Mgogoro wa nafsi kwa Sekai. Sekai alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kwa muda mrefu juu ya mwanae ambaye alitengwa na kubezwa kutokana na hali yake. Alilia na kuhuzunika mara nyingi akiilaumu Miungu yao kuwa “Sisi tumefanya nini” hatimaye mgogoro wake uliisha baada ya Takadini kujenga heshima yake upya mara alipomuoa Shingai na kubahatika kupata mtoto wa kiume tena asiye Sope. Na hapo ndipo ilirejea faraja na furaha mpya.
Mgogoro wa nafsi kwa Takadini: Huu ulisababishwa na hali yake ya ulemavu wa ngozi iliyopelekea yeye kutengwa na kubaguliwa na wanajamii na mara kadhaa kutishiwa kuuawa. Hali hii ilimtesa ka muda mrefu kwani alitengwa na hakuwa na rafiki toka utotoni hadi ujana wake. Lakini mgogoro huu unaisha baada ya kupata mke aliyempenda kwa dhati na kumzalia mtoto wa kiume. Hii inampa faraja na kujiona mwanaume halisi na kuithibitishia jamii kuwa alikuwa sawa na wanajamii wengine.
FALSAFA: Falsafa ya mwandishi Ben Hanson, anaamini kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama binadamu wengine kwani wana akili, utashi, uwezo wa kufanya kazi kama binadamu wengine na ni sawa na binadamu wengine.Wao kuwa na ulemavu wa ngozi si kigezo cha kuwaua na kuwabagua. Hana imani juu ya mila potofu kwani katika masimulizi yake anaonesha kushindwa kwa mila potofu kama vile kuamini kuwa albino ni viumbe waliolaaniwa na hawatakiwi kuishi. Anaamini kuwa wakipewa nafasi ya kuishi na kushirikishwa katika shughuli za kijamii, kupewa elimu na mahitaji yote wanaweza kuwa ni watu muhimu sana katika jamii na hili analidhihirisha kupitia Takadini.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Tunaweza kusema hivyo kwa sababu ya mambo ambayo mwandishi anayamulika katika kazi yake. Mambo kama vile kuzaliwa kwa albino haoni kuwa ni laana bali ni kawaida tukutokana na masuala tu ya kimaumbile. Haoni kuwa kuna haja ya kuwatenga au kuwabagua albino kwakuwa ni binadamu sawa na sisi.
MSIMAMO: Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi kwani analenga kuyapindua mawazo na imani potofu za baadhi ya jamii kuwa albino hafai kuishi. Anakemea suala la kuwatenga na kuwabagua albino, anakemea pia suala la ndoa za lazima na mila zingine potofu. Anataka jamii ibadilike na kuendana na wakati kuwapa usawa watu walio na ulemavu wa ngozi, anatetea haki za wanawake anataka wapewe nafasi sawa katika jamii wasibaguliwe. Hivyo msimamo wa mwandishi ni mzuri na unatakiwa kufanyiwa kazi katika jamii.
FALSAFA
Kupitia Takadini, Mwandishi amwonyesha falsafa zifatazo
Mwandishi anaamini hata mtu mwenye ulemavu wowote wanaweza kupata nafasi katika jamii kwa kumtumia muhusika mkuu takadini
Mwandishi anaanimi wapo wanawake ambapao bado hawana maamuzi kuhusu ndoa zao,kwa sababu wanachaguliwa wachumba/ wanaumw kwa mtumia
Mwanadishi anaamini kuwa mila mbaya za kiafrika zinabidi ziondolewe.
Mwandishi anaamini elimu ndio chanzo kizuri cha waelewano katika jamiii,kwa sababu wapo watu wanafanya wafanya mambo kwa sababu ya kukosa elimu.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwa kutumia kitabu hiki tumepata mitazamo mbalimbali kama ifatavyo,
Mwandishi anaona kuwa hata mtu mwenye ulemavu wowoteanaweza kupata nafsi katika jamii,kwa kumtummia muhusika mkuu takadini
Mwandishi anaona kuwa mila mbaya za kiafrika zinabidi ziondolewe
Mwandishi anaona elimu kuwa ndio chanzo kizuri cha maelewano katika jamii husukia
MSIMAMO: Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi kwani analenga kuyapindua mawazo na imani potofu za baadhi ya jamii kuwa albino hafai kuishi. Anakemea suala la kuwatenga na kuwabagua albino, anakemea pia suala la ndoa za lazima na mila zingine potofu. Anataka jamii ibadilike na kuendana na wakati kuwapa usawa watu walio na ulemavu wa ngozi, anatetea haki za wanawake anataka wapewe nafasi sawa katika jamii wasibaguliwe. Hivyo msimamo wa mwandishi ni mzuri na unatakiwa kufanyiwa kazi katika jamii.
UJUMBE
Albino au watu wenye ulemavu wa ngozi wanatakiwa kupewa haki ya kuishi, kupendwa kusaidiwa na kulindwa.
Mila na desturi potofu si budi kupigwa vita katika jamii.
Upendo na huruma ni mambo ya msingi katika jamii.
Wanawake wapewe uhuru wa kuchagua wanaume wanaowapenda kuishi nao katika ndoa.
Wanawake wapewe nafasi na kushirikishwa katika masuala ya jamii.
Malezi bora ni msingi wa jamii na taifa kwa ujumla

Maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
Hakiki maudhui katika Riwaya ya Joka la Mdimu
DHAMIRA
Ugumu na hali ngumu ya maisha:Suala la ugumu wa maisha limejadiliwa katika riwaya hii kwa kiasi chake. Mwandishi ameonesha jinsi wananchi wanavyopata shida ya vyakula, mavazi nk. Yote haya yakisababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa kutokana na uhaba wa bidhaa. Mfano. Uk.1“jiji la Mindule lilikabiliwa na uhaba mkubwa mno wa petroli, dezeli na mafuta ya taa nyumba nyingi zisizo na umeme zilibaki kiza usiku maana mishumaa ilikuwa ghali na adimu kupatikana, usafiri ulisimama isipokuwa kwa wale wachache waliojua mbinu za kupata dizeli na petrol”.Mwandishi ameonesha jambo hili ambalo linaakisi maisha ya hali ya kiuchumi miaka ya 80, ambayo kwa upande mwingine inaangazia maisha ya mtanzania wa leo ambapo bidhaa ni nyingi maasokoni lakini tatizo ikiwa ni mfumuko wa bei na upatikanaji mgumu wa fedha.
Suala la utabaka:Utabaka uliojadiliwa ni kati ya walionacho na wasionacho (matajiri na maskini). Hili limeoneshwa pale ambapo wananchi wanaishi maisha ya dhiki na makazi duni mfano uk.29 mwandishi anaeleza,“nyumba yenyewe ya Tino ilikuwa bondeni juu tu kidogo ya mtaro mkubwa uliokuwa ukipitisha maji machafu”.Hii inatuonesha wazi hali mbaya ya makazi ya Tino na wakazi wengine, wakati hawa maskini wakiteseka na kuhangaika hata katika suala la huduma za kijamii kama matibabu ya gharama kubwa, matajiri wao walinufaika kwa kuwa na fedha nyingi, mali za kujilikimbikizia na za magendo. Mfano uk. 103 – 104 mwandishi anaeleza kuhusu makazi au nyumba ya Brown“ilisimama na kuzibeza nyumba zote jirani na hapo kwa haiba yake na bwawa lake la kuogelea”.
Ufisadi: Suala la ufisadi limeoneshwa na mwandishi kwani amejadili kuhusu viongozi ambao wanahujumu mali za umma kwa maslahi yao binafsi, viongozi mfano wafanyakazi wa serikali kama vile Brown Kwacha amechorwa kuwa ni mtumiaji mbaya wa mali za umma, anasafiri safari za nje kwa pesa nyingi za serikali na kwa matumizi binafsi. Licha ya hivyo anafanya biashara ya magendo na pesa za kigeni katika ofisi yake. Alimudu kujenga nyumba za kifahari kwa pesa za serikali. Mfanouk.102“gharama ya nyumba iliyokuwa ikijengwa na Wafaransa ilikuwa shilingi milioni mia mbili na nusu na ile nyingine milioni mia tatu”.Hizi ni pesa nyingi ambazo zote alizichukua serikalini.Hili ni tatizo kubwa kwa jamii yetu ya leo. Viongozi wetu wa serkali wanatumia pesa vibaya za serikali kwa manufaa binafsi, hivyo kusababisha umaskini usioisha kwa Watanzania wa hali ya chini. Mwandishi amelionesha hili ili wanaohusika wabadilike.
Biashara haramu na uharibifu wa mali za taifa:Suala hili limejadiliwa katika riwaya hii. Mhusika Brown ambaye ni mfanyakazi wa serikali anajihusisha na biashara za magendo mfano uuzaji na uwindaji wa wanyama na kuchukua pembe, ngozi na meno. Mfano uk.122-123 muwindaji kinara wa Brown anasema“sawa ziko pembe ishirini za faru na sitini za ndovu, unaweza kuzichukua zote maana vitu hivi ni hatari”.Wanyama muhimu katika hifadhi za taifa wanazidi kupungua na kutoweka kabisa kutokana na biashara hii. Mwandishi ameliangazia ili mamlaka husika na jamii viweze kuweka mikakati na sheria madhubuti za kuangamiza suala hili kwani hupelekea nchi kuendelea kuwa maskini.
Rushwa na kutowajibika:Mambo ya hongo na rushwa na kutowajibika kwa viongozi ambao wamepewa mamlaka na wananchi ili wafanye kazi kwa maslahi ya taifa yamejadiliwa. Mfano mhusika Brown si mfanyakazi bora kwani hakutimiza wajibu wake bali alifanya kazi kwa upendeleo mkubwa bila kujali haki. Alipokea rushwa na kutoa pia. Mfano uk.100 anasema“……lakini Brown Kwacha alikuwa mtu wa nyendo akajua karata gani acheze na ipi aibakishe. Alisema kwa kiburi suala si kupata kiwanja ila mahali panapofaa kuporomoshwa kasri la kifahari”. Hivi ndivyo hali ilivyo, wenye uwezo wa kutoa rushwa ndio waliopatiwa huduma haraka. Pia anatuonesha jinsi Brown Kwacha alivyofanya kazi kwa upendeleo uk.97 mwandishi anasema “katibu wa Brown Kwacha alimtazama mkuu wake wa kazi akastaajabia namna alivyoweza kukaidi kuwahudumia wengine ila alivyolainika mbele ya wasichana kama jani la mboga au bufalo ndani ya maji.” Suala hili ni tishio kwa Wananchi kwani hupoteza wa haki, mwandishi anakemea suala hili vikali, na viongozi wanashauriwa kuenenda kwa mujibu wa maadili ya kazi zao.
Mapenzi: Mapenzi aliyoyajadili mwandishi katika riwaya hii ni ya sura mbili tofauti.Mapenzi ya dhati;Hili limeoneshwa na mhusika Amani kwa rafikiye Tino, kwani alibeba suala la Tino kuuguliwa na mwanae kama lake, alimsaidia katika shida na raha, hakumuacha peke yake mfano uk.145. mwandishi anasema Tino akawaza“akawaza dunia hii ya leo nani atajitoa kwa hali na mali kumsaidia kapuku kama yeye. Nitamlipa nini Amani?”hii inaonesha fadhila alizokuwa nazo Amani. Pia mapenzi ya dhati yameoneshwa kwa Tino kwa mwanae Cheche na familia yake. Tino aliipenda sana familia yake hata kuhangaika kwa hali na mali kumtibu mwanae Cheche kwa kila gharama kwani alidiriki kuiba fedha benki ili amudu kumpeleka mwanae nje kwa ajili ya matibabu. Mwandishi anatufundisha kuwa na mapenzi ya dhati kwani ni ishara ya mafanikio na amani. Kwa upande wa pili amejadili juu ya mapenzi yasiyo ya dhati au ya kweli. Mhusika Brown amechorwa kutokuwa na mapenzi ya dhati na kukosa uaminifu kwa mkewe na watoto kwani ni muhuni sana. Alikuwa na mahusiano ya mapenzi na wanawake wengi hakujali familia yake kabisa. Hakuonesha hata chembe ya upendo kwa familia yake. Mfano uk.109“mabinti zake walitamani sana kusafiri na baba yao. Lakini licha ya safari zake nyingi mno hawakupata fursa hiyo.”Pia uk.106 anasema watoto walikosa upendo“walitapia mno, lau kungekuwa na maelewano na upendo mkubwa baina ya baba na mama yao!fauka ya hayo baba yao alikuwa mkali”.Pia mapenzi yasiyo ya uaminifu kwa Brown na wapenzi wake kama vile Leila, Josephine. Mapenzi haya yalikuwa ya pesa tu! Uk 112 mwandishi amemzungumiza Leila “badala ya kumfikiria zaidi Brown Kwacha akatarajia zaidi faraja kuangalia nwanyama kwenye hifadhi ya Kwale”.Piauk.99Josephine anaomba fedha kwa Brown“.. cha kutosha kununua vitu vya harusi kama paundi alfu sita hivi”Mapenzi yasiyo ya dhati na ukosefu wa uaminifu katika ndoa ni janga katika jamii za sasa kwani wazazi hujisahau na kukiuka maadili ya ndoa jambo ambalo ni hatari mno kwani husababisha migogoro na ugomvi katika familia (mafarakano) na hata kuambukizana magonjwa hatari.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Amechorwa kama chombo cha starehe: Mfano ni Josephine na Leila, Brown Kwacha aliwatumia kujiburudisha kwa uasherati, pia wanawake walijiuza katika moja ya sehemu ambazo Amani alipenda kwenda.
Amechorwa kama kiumbe mwenye upendo: Mwema mke wa Tino ni mwanamke ambaye alikuwa na upendo wa dhati kwa mumewe na watoto kutokana na matunzo aliyowapa.
Amechorwa kama mlezi: Mfano mzuri ni Mwema na mke wa Brown ambaye yeye alikuwa ndiye mwangalizi mkuu wa familia kwani mumewe hakuwa na muda huo zaidi ya kuponda starehe na anasa kwa mda wa ziada aliopata badala ya kukaa na familia yake.
Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mke wa Brown alivumilia sana mateso ya mmewe, hakuamua kumuacha bali alivumilia pamoja na kumdharau kote, kumdunisha na kutomthamini kama mke.
Amechorwa kama kiumbe duni: Brown hakumshirikisha mkewe katika maamuzi yoyote yale wala hakutaka ushauri wowote kutoka kwake alimdharau na kumpuuza tu.
Kama mtu jasiri na mwenye msimamo: Pamela anaoneshwa kuwa ni mwanamke jasiri kwani aliweza kumkataa Brown kimapenzi pamoja na vishawishi vya kila aina. Mfano uk.99 mwandishi anasema“lakini Pamela kama mwanariadha stadi, aliviruka viunzi vyote vya Kwacha…… mwanzo alimchukia lakini taratibu alianza kumheshimu”.
MIGOGORO
Mwandishi Safari pamoja na kujenga visa vyake vya kusisimua pia hakuacha kuibua migogoro ili kukamilisha masimulizi ya visa vyake.
Mgogoro baina ya pande mbili
Mgogoro baina ya Josephine na mke wa Brown: Sababu ya mgogoro huu ni Josephine kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na Brown Kwacha na kufumaniwa na mke wa Brown. Walipigana na kuumizana lakini Josephine hakuacha mahusiano hayo.
Mgogoro kati ya wafanyakazi wawili wasukuma makwama: Sababu ya mgogoro huu waligombaniana matenga ya kubeba na mwishowe kuishia kupigana.
Mgogoro baina ya Jinja Malon na vibaka: Jinja Malon aliwapiga vibaka baada ya kutaka kumkwapulia mwanamke mmoja hereni, mkufu na hata kutaka kumbaka kichochoroni. Uk 51-52.
Mgogoro kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya mila na utamaduni na kijana mmoja:Walipigana kugombania mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na wanawaume wote wawili. Uk.102.
Mgogoro wa nafsi wa Tino
Tino alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kutokana na hali ya ugonjwa wa mwanae Cheche. Hakujua apate wapi pesa za kumtibia kwani hakuwa na pesa na alitakiwa kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu. Lakini baada ya kushauriwa na Amani akaibe pesa alifanya hivyo na kufanikiwa na ndipo alipata amani baada ya kumudu gharama za matibabu ya mwanae.
FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa chanzo cha matatizokatika jamii ni upotofu wa maadili, kutowajibika, mifumo mibovu ya uchumi, rushwa, ufisadi na biashara haramu na mengine mengi. Anaamini kuwa endapo jamii itabadilika basi hayo matatizo hayatakuwepo. Anatoa suluhu ya matatizo hayo kama vile kupinga utabaka, rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka na kuwa na usimamizi mzuri wa mali za umma.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Ameonesha matatizo ndani ya jamii na kuonesha suluhu ya matatizo hayo. Anaonesha matatizo ya uhujumu uchumi, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi, ukosefu wa huduma za jamii, matabaka na hali ngumu ya maisha. Anaona kuwa sababu ya matatizo haya si ya kidhanifu tu au ni mipango ya Mungu tu! Ila anonesha sababu za matatizo hayo kama vile kukithiri kwa rushwa, mifumo mibaya ya kiuchumi na anatoa suluhu kwa kuwapiga vita viongozi wasowajibika. Mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kutengeneza utabaka katika jamii.
MSIMAMO: Mwandishi A. Safari ana msimamo wa kimapinduzi, hili linajidhihirisha wazi kutokana na mambo anayoyaeleza ambayo yanalenga kuibadili jamii. Analeta mapinduzi kwa viongozi wasiowajibika, mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kusababisha umaskini na kuwakweza wachache.Anatoa suluhu ya matatizo mbalimbali. Anakemea malezi mabaya kama ya Brown pia anasa na starehe na mengine mengi.
UJUMBE
Viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kulingana na majukumu yao.
Rushwa, ufisadi na biashara za magendo ni vikwazo vya maendeleo hivyo si budi kupigwa vita.
Serikali na mamlaka husika vinapaswa kusimamia vyema sheria na taratibu ili kuwawajibisha wanaoenda kinyume kama vile wahujumu uchumi.
Uaminifu katika ndoa na mapenzi ya dhati ni jambo la msingi kwani huongeza Amani katika familia.
Jamii inapaswa kutambua nafasi ya mwanamake na kumshirikisha na sio kumdunisha bali apewe nafasi ya kuamua na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaedeleo.
Uhakiki wa Maudhui katika Tamthiliya
Maudhui katika Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
DHAMIRA
Dhamira kuu
Suala la kuchanganya kazi na mapenzi: Mhusika Ngoswe ambaye alitumwa na serikali kwenda kufanya zoezi la sensa la sensa kijijini anajiingiza katika mapenzi na binti Mazoea uk.5 na hivyo kusababisha kutokuwa makini na kazi yake. Anaamua kutoroka na Mazoea jambo ambalo linamfanya Mzee Mitomingi ateketeze karatasi za takwimu kwa kutoroshewa mwanae uk.28. hivyo tunaona jinsi mapenzi yallivyohaaribu kazi.Suala hili ni halisi katika jamii yeetu ya leo kwani watu wamekuwa wakijisahau na kuchanganya kazi na mapenzi, mwandishi ameliweka jambo hili wazi ili jamii iweze kubadilika na kuacha tabia hiyo mbaya inayodidimiza maendeleo ya jamii.
Dhamira ndogo ndogo
Hasara za ulevi: Suala la ulevi na hasara zake limejadiliwa na mwandishi akiwachora wahusika kama Ngoswe na Mzee Mitomingi na wanakijiji ambao ni walevi. Mfanouk.6 Mzee Mitomingi anasema “haya matatizo yote ni shauri ya pombe, sina shaka yuko kilabuni”.Ngoswe naye anapata hasara kutokana na ulevi kwani analewa sana na kuchoma karatasi za takwimu na kusababisha kuhesabu upya watu tena jamo ambalo lilipoteza mda zaidi.uk.18-19.Katika jamii yetu suala laulevilina hasara kubwa kama vile kurudisha nyuma suala zima la maendeleo, kusababisha vifo na ajali, migogoro ya kifamilia na matatizo mengine mengi. Jamii inaaswa kujirekebisha na kukemea suala hili kwani lina madhara makubwa katika koizazi cha sasa.
Umuhimu wa elimu: Wanakijiji wa kijiji cha Mzee Ngengemkeni hawana elimu na wala hawatilii maanani juhudi za kupata elimu. Huduma za kielimu ni mbovu kama vile shule iko mbali sana hazipo kijijini kwao. Familia nyingi na watoto wao hawasomi. Uk.16. zoezi la uhesabuji watu linakuwa gunu zaidi kuutokana na watu kutokuwa na elimu.Ili kupata maendeleo katika jamii yoyote ile si budi suala la elimu kupewa kipaumbele na wanaoelimika wanapaswa kutumia vyema elimu yao. Wanapaswa kurejesha mchango chanya katika jamii na sio kurudisha nyuma maendeleo.Mfano Ngoswe ambaye hakutumia vizuri elimu yake. Elimu lazima itumike kuibadilisha jamii na kusukuma mbele zaidi maendelo.
Suala la umaskini: Wanakijiji wanaelezwa kuwa na maisha duni sana ya hali ya chini, makazi duni. Mfano wanalala kwenye vibanda vibovu mfano Ngoswe anakaribishwa kulala katika moja ya kibanda kibovu kinaachovuja. Mwandishi amelionesha hilo makusudi kwani maeneo mengi ya mijini yamesahaulika na bado wapo nyuma kimaendeleo. Serikali iangazie maeneo ya vijijini na kutoa elimu ya namna ya kupambana na umaskini, kujenga makazi bora. Pia wanakijiji wanaaswa kuacha uvivu na kujishughulisha ili kumpinga adui maskini.
Suala la malezi na ndoa za mitara: Wanakijiji wa Balozi Mitomingi wana utamaaduni wa kuoa mke zadi ya mmoja. Pia suala la malezi si la baba bali la mama pekee. Mzee Mitomingi aliwaachia wakeze suala la kulea watoto na kuwa watazamaji wa familia, hali kadhalika Mzee Jimbi mda wote alishinda kilabuni kwenye pombe na hakuwa na mda wa kufanya kazi yoyote ya kimaendeleo wala kuangalia familia suala hilo aliwachia wake zake. Hili si jambo zuri.Kuhusu ndoa za mitara kwa jamii ya leo zina athari kwanikatika malezi ni vigumu kumudu ukubwa wa familia, usalama wa kiafya huwa ni mdogo kwani wanandoa wana hatari kubwa ya kuambukizana magonja hatari.
Imani potofu na ushirikina: Uk.14 tunaona wanawake wanakataa zoezi la kuhesabiwa kutokana na imani kuwa mtu anayehesabu watu ni mchawi. Kutokana na hili, zoezi la uhesabuji watu linakuwa gumu.Wanaamini kuwa mtu akifa basi amerogwa. Mfanouk.16 “wamemroga bure mume wangu. alikufa akiwa na nguvu zake”.Mambo mengine ya kimaendeleo hushindikana kutokana na imani potofu wanazoshikiliawanajamii. Mwandishi amelionesha ili jamii ijikomboe kutoka katika imani hizo potofu. Pia anaona upo umuhimu wa serikali kuelimisha jamii juu ya hili, kuacha kushikilia ukale na kuchangamkia maendeleo.

Utabaka kati ya mjini na vijijini:Katika tamthiliya hii suala la utabaka kati ya mjini na vijijini. Kuna tofauti kubwa kati ya mjini na vijijini katika masuala ya huduma za jamii kama vile elimu, afya na mengineyo. Uk.29 Ngoswe anasema:“Shurti vijiji kurekebishwa,Ujinga, magonjwa naUmaskini kupigwa vita,Na njia ni moja tu!Kuishi pamoja kijamaa.”Hivyo mwandishi amelionesha jambo hili ambalo linahalisika katika jamii yetu ya leo, hivyo si budi serikali kulitazama jambo hili kwa jicho pevu. Teknolojia na mawasiliano yaboreshwe kwani ni msingi wa maendeleo.
Nafasi ya mwanamke
Tamthiliya ya Ngoswe imemchora mwanamke katika sura zifuatazo:
Kama mlezi na muangalizi wa familia: Mama Mazoea na mama Inda na akina mama wengine ni waangalizi wa familia.
Kama chombo cha starehe: Wanaume wameonekana kuwatumia wanawake kwa ajili ya starehe. Hii inathibitishwa na tabia ya kuoa mitara.
Kama kiumbe duni asiyeweza kutoa maamuzi yoyote ndani ya jamii yake: Mfano Mitomingi anasemauk.26 “nyie wanawake akili zenu wote sawa si Mazoea si mama yake….”Jamii inashauriwa kumpa mwanamke nafasi na kumthamini hasa katika masuala ya uamuzi.
Kama mtu asiye na msimamo: Mfano ni Mazoea ambaye anaamua kutoroka na Ngoswe huku alijua ametolewa mahari.
MIGOGORO
Mgogoro kati ya Ngoswe na Mzee Mitomingi: Mgogoro huu unatokea baada ya Ngoswe kuamua kumtorosha binti wa Mitomingi. Mitomingi anaamua kuchoma moto karatasi za takwimu.
Mgogoro baina ya Mazoea na wazazi wake: Sababu ya mgogoro ni Mazoea kujihusisha na mapenzi na kutoroka na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari. Baba yake alimuadhibu kwa kumchapa.
Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali: Sababu ya mgogoro ni kutokana na Ngoswe kushindwa kupeleka hesabu ya watu kama alivyoagizwa. Uk.28-29.
Mgogoro wa nafsi wa Ngoswe. Ngoswe alisononeka na kuwaza kuwa angejibu nini serikalini kwani karatasi za takwimu ziliteketea kutokana na uzembe wake.
FALSAFA: Imani ya mwandishi anaamini kuwa mabadiliko na maendeleo katika jamii yanawezekana kama watu watajishughlisha na pia kama serikali itagawanya vyanzo vya maendeleo bila ubaguzi nchini. Pia anaamini kuwa jamii inaweza kuingia matatizoni kama itachanganya mambo mawili kwa pamoja. Hivyo anashauri watu kuheshimu na kushikilia jambo moja ndipo utafanikiwa.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani anayaona mambo kiyakinifu, anaona kuwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu kazi, kuwa na msimamo katika maisha ni suluhisho na chachuya maendeleo.
MSIMAMO: Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani anapingana na mambo mabaya na kuyaweka wazi mfano uvivu, uzembe, kuchanganya kazi na mapenzi. Pia anapinga suala la ushirikina na imani potofu. Anaona kuwa ipo haja jamii kuwa na msimamo wa kimapinduzi kwa kupinga mambo yanayodidimiza maendeleo.
UJUMBE
Si vyema kuchanganya kazi na mapenzi kwani husababisha kazi kuharibika.
Ulevi huleta madhara na matatizo ndani ya jamii hivyo si budi jamii kupinga ulevi.
Elimu ni muhimu sana kwa jamii yoyote.
Kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa maendeleo.
Wanawake wanapaswa kupewa nafasi ya kufanya maamuzi katika jamii.
Serikali na jamii vinapaswa kugawanya maendeleo sehemu zote za vijijini na mijini ili kuwa na maendeleo yasiyopishana sana ili kufifisha umaskini uliokithiri.
Wanaume wanaowavuruga wasichana kwa tamaa zao ipo siku watafikia tamati na kupata machungu ya ubaya wao.
Msimamo katika maamuzi ya mambo na kufikiri kabla ya kutenda ni jambo la msingi.
Nidhamu ya woga haijengi.

Maudhui katika Tamthiliya ya Kilio Chetu
Hakiki maudhui katika tamthiliya ya Kilio Chetu
DHAMIRA
Athari za gonjwa la ukimwi. Suala la ugonjwa wa ukimwi na athari zake limeajadiliwa katika kitabu hiki. Vijana wadogo kama Joti anaathirika na gonjwa hili kutokana na ukosefu wa elimu ya jinsia na magonjwa. Mwandishi anaelezea dalili,jinsi na ueneaji wa ukimwi jinsi ulivyo,pia athari za zake na namna ya kuwatunza wagonjwa wa ukimwi. Suala hili limekumba jamii yetu kwa kiasi kikubwa, mwandishi ananafananisha janga hili na dubwana uk.1. Jamii yetu ya sasa inaapaswa kuwakinga vijana wadogo na mambukizi haya kwa kuwaelimisha zaidi na kuwaasa bila kuwaonea haya.
Elimu ya jinsia: Elimu ya jinsia imejadiliwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa kizazi cha leo, kinachokumbwa na mabadiliko makubwa ya kijamii hususani utandawazi. Kijana Ana alipatiwa elimu ya jinsia na ikamsaidia katika kupambana na vishawishi. Uk.25. hii ni kinyume na kwa mtoto Suzi na Joti, Mwarami na wengine ambao hawakubahatika kupata elimu hiyo. Wanaishia kupata madhara makubwa mfano Joti anakufa kwa ukimwi na Suzi anapoteza masomo kwa kupata ujauzito. Jamii haina budi kutoa elimu ya jinsia kwa vijana bila aibu kwani ndio mkombozi wa maisha ya ujana yenye changamoo nyingi, na tusiwe kama mama Suzi anaposemauk.9 “tena ishia hapohapo kaka! Huko si ndiko mkunifundishia mwanangu habari za ngono ilitoka wapi hiyoo….?”Hakubaliani kabisa kutoa elimu ya jinsia kwa mwanae kwani anaona ni kama uchuro na kufumndisha uhuni.
Mapenzi katika umri mdogo. Vijana wadogo hawapaswi kushiriki katika mapenzi mpaka pale wanapokuwa tayari. Kilio chetu kimejadili na kuonesha jinsi vijana wadogo Joti na Suzi wanavojiingiza katika ngono jambo ambalo ni kinyume na maadili yetu. Uk.16-17, 19-21. Si hivyo tu bali wanajiingiza katika mapenzi mpaka na watu waliowazidi umri mfano mwandishi anamsemea Jotiuk.23“sasa ndiyo kuparamia mpaka wasichana wakubwa wa mitaani? Fikiri juu ya Chausiku yule msichana mjuvi wa mji ambaye pia anachukuliwa na yule Mpemba muuza duka”Vijana wanaaminishana kuwa mapenzi ni halali yao, mfano uk.22 Jumbe anasema“MAPENZI NI TIBA”.Si budi jamii kukemea suala hili vikali kwani hupoteza nguvu kazi ya taifa la leo na kesho.
Athari za utandawazi. Masuala ya intaneti, sinema na picha za ngono, leo hii zina madhara mabaya kwa vijana wetu. Hutolewa bure bila kizuizi chochote wala hamna taratibu zozote zile zinazowabana watoto kuangalia mambo hayo. Vijana wa sasa wamekuwa wakipoteza mda mwingi na hata kufeli katika masomo yao kutokana na hili. Jumbe anasemauk.17 “leo si ndio siku ya picha ya “X”? umesahau?”.Ipo sababu sababu ya msingi kwa jamii kutafuta namna ya kuwaokoa vijana na kuweka taratibu zitakazowalinda juu ya hili.
Suala la malezi: Malezi bora yanayozingatia maadili ya jamii husika ni jamo la msingi sana. Jamii nzima inapaswa kushiriki katika malezi ya watoto.Katika kitabu Mama Ana na Baba Ana na Mjomba wameonesha mfano bora wa wazazi wazuri mfanouk.11 mjomba anasema “mzazi ndiye mwalimu wa kwanza” pia Baba Ana anasema “….mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu”Hivyo tunaona kuwa mzazi ndio msingi wa maadili mema kwa mtoto, wazazi wanaaswa kuwa makini zaidi katika malezi.
Mapenzi na ndoa. Mapenzi na ndoa zimejaa udanganyifu na ulaghai siku hizi kwani uaminifu limekuwa jambo gumu ka wanandoa mfano uk.6-7 Mama Joti anaonesha wasiwasi wa kuchukuliwa mume wake na wanawake wengine anasema“huu ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu Nguru anayeichimba ndoa yangu”.Hii inaonesha wazi suala la wanandoa kuwa na wapenzi wengine nje ya ndoa ni tatizo kwa jamii. Mwandishi amelionesha hili makusudi ili jamii iepuke haya kwani huleta madhara makubwa katika familia na jamii kama vile kutojali familia, kuambukizana magonjwa hatari na hata mafarakano ya wazazi.
Mila na desturi potofu. Mila na desturi potofu zikiendelea kushikiliwa na jamii yetu ya leo ni tatizo kwani zinasababisha madhara. Tunamuona Mama Suzi ambaye anaona suala la kumuweka wazi mwanae kuhusu mambo ya ukuaji, mapenzi na athari zake ni gumu. Anasemauk.10 “mie nikae hapa nafungua kinywa changu (anaigiza): sasa mwanangu mafanye hivi na vile…. Na vile mimba itatokea… uchuro huo!”.Anaona suluhisho ni kumpiga tu pale atakapokosea, jambo ambalo si sahihi kabisa kumbe tunapswa kuzitupilia mbali na kuendana na mabadiliko yenye tija kwa jamii yetu.
Huduma kwa wagonjwa wa UKIMWI. Hii pia ni dhamira muhimu iliyojadiliwa katika tamthiliya hii kwa jamii. Jamii ya sasa yenye watu waaathirika na gonjwa hili sekta na asasi mbalimbali zinatoa ushauri wa namna ya kuwatunza wagonjwa hawa.Mwandishi amelionesha hili ili jamii iwapende, kuwajali, kufurahi pamoja nao na kutowatenga kabisa. Faraja na matumaini ni jambo la msingi kwa wagonjwa wa Ukimwi, mfano uk.11 maelezo ya Mjomba juu ya kumtunza mgonjwa.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Amechorwa kama mtu mwenye msimamo na tabia njema: Mfano mzuri ni Ana. Aliweza kupinga vishawishi na aliwaelimisha wenzake juu ya elimu ya jinsia.
Amechorwa kama muelimishaji: Mama Ana ni mwanamke ambaye anatambua umuhimu wa elimu ya jinsia na alielimisha vyema, mfano mwanae Ana alikuwa na tabia njema na alifanikiwa.
Kama mtu muhuni: Msichana Chausiku alikuwa na wanaume wengi na tamaa, kwani aliweza hata kuwa na mahusiano na kijana mdogo Joti.
Mtu asiyependa mabadiliko (anayeshikilia mila na desturi potofu): Mfano mzuri ni Mama Suzi anashikilia mambo ya zamani, hataki kumuweka wazi mwanae Suzi kuhusu masuala ya jinsia, mapenzi na athari zake. Hafai kuigwa na jamii.
Kama kiumbe duni asiye na kauli (mwoga). Mama Joti alishindwa kuwa muwazi kupigania ndoa yake iliyovamiwa na wanawake wengine, bali anapitia njia za pembeni kutatua taizo hili kama vile kununua na kuvaa kanga zenye maandishi ya kejeli kumsema mwanamke anayemuibia bwana wake.
Kama mlezi bora wa familia. Mama Ana alishiriki kikamilifu katika malezi ya bintiye Ana na kumuokoa toka katika wimbi la vishawishi na maradhi, mimba za utotoni na matatizo mengine. Anafaa kuigwa na jamii kwani ni mfano bora.
MIGOGORO
Mgogoro kati ya Suzi na Mama Suzi. Mama Suzi alimwadhibu Suzi kwa kipigo baada ya kukuta Suzi akiwa na vidonge vya kuzuia mimba kaika mfuko wa sare za shule. Hii haikuwa suluhisho bora la mgogoro huu.
Mgogoro kati ya Joti na Chausiku. Sababu ya mgogoro huu ni Joti kuwa na mahusiano na Suzi ilihali pia alikuwa na Chausiku. Suluhisho Chausiku anamuonya Joti achane na Suzi.
Mgogoro kati ya Suzi na Joti. Sababu ya mgogoro ni Suzi kukataa kuendelea na mahusiano na Joti baada ya kugombezwa na mama yake. Suluhisho la hili Suzi anaamua kuendelea na mahusiano hayo baada ya ushawishi kutoka kwa Joti alihofia kumpoteza Joti.
Mgogoro wa nafsi wa Suzi: Suzi alijuta na kuwaza juu ya maisha yake. Alijihoji maswali yasiyo na majibu kuwa je alikuwa ameambukizwa virusi na Joti? Alikuwa pia haaamini kuwa tayari ana mimba alijihoji nafsi yake na kulia. Hakuwa na suluhu ya mgogoro huo zaidi ya kurudisha lawama kwa mama na jamii yake ambao hawakumuelimisha juu ya magonjwa na athari za mapenzi katika umri mdogo.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu,katika kazi ya uhakiki mwandishi lazima awe na mtazamo maalumu ambao unagusa jamii husika au tabaka tawala,katika tamthilia hii mwandishi ameonyesha mtazamo mkuu na mitazamo ya kawaida.
Mtazamo mkuu
Mwandishi anaona kuwa ugonjwa wa ukimwi ni hatariMitazamo midogo midogo Mwandishi anaona mapenzi na shule ni vitu ambavyo haviendani
FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa endapo vijana na watoto wataelimishwa kuhusu elimu ya jinsia wataokoka toka katika wimbi hatari la magonjwa na mmonyoko wa maadili. Haamini juu ya imani poofu kwani anazipinga kwa kuonesha ukweli na uhalisia wa mambo yalivyo mfano haamini kuwa ugonjwa wa ukimwi hupatikana kwa kurogwa ila kupitia kujamiiana na muathirika au kuchangia vyombo vyenye ncha kali au hata akuongezewa damu yenye virusi. Ila anaamini kuwa njia hatari zaidi ni kujamiiana hivyo anaiasa jamii kuepuka.
MSIMAMO: Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi, mambo anayoyakemea na kuyapinga yanalenga kuibadilisha jamii kutoka katika ukale na kushikilia mila potofu. Anaipinga tabia ya wazazi wasiotaka kuwa wazi kwa watoto wao na kuwaelimisha juu ya mabadiliko ya jamii yanayokumbwa na magonjwa hatari, utandawazi na mengineyo.
UJUMBE
Wazazi wanapaswa kutoa malezi bora kwa watoto wao.
Elimu ya jinsia ni muhimu kwa vijana na wazazi
Elimu ya ukimwi ni muhimu kwa jamii
Mila na desturi potofu si budi kupigwa vita
Uaminifu katika ndoa ni jambo jema
Mapenzi katika umri mdogo ni sumu
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu,katika kazi ya uhakiki mwandishi lazima awe na mtazamo maalumu ambao unagusa jamii husika au tabaka tawala,katika tamthilia hii mwandishi ameonyesha mtazamo mkuu na mitazamo midogo midogo.
Mtazamo mkuu
Mwandishi anaona kuwa ugonjwa wa ukimwi ni hatari
Mitazamo midogo midogo
Mwandishi anaona mapenzi na shule ni vitu ambavyo haviendani.
Mwandishi anaona kusikiliza wazazi ni kitu kizuri.
Mwandisi anaona hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho katika jambo baya lolote unalotenda.
FALSAFA
Falsafa kuu
Falsafa za kwaida
Mwanidishi anaamini kuwa urafiki mbaya ni chanzo cha matatizo
Mwandishi anaamini kuwa elimu ndio ukombozi wa jamii
wandishi anaamini kuwa matatizo ya kifamilia yamalizwe na familia husika kwanza,
Maudhui katika Tamthiliya ya Orodha
DHAMIRA
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi
Hii ni dhamira kuu iliyojadiliwa katika tamthiliya hii. Mwandishi analenga katika mapambano ya Ukimwi hasa katika maeneo ya vijijini ambapo bado elimu kuhusu ugonjwa huu haijafika vyema. Anamtumia mhusika Furaha kutuonesha jinsi binti huyu mdogo wa kijijini anavopata ugonjwa huu na hatimaye kufa. Furaha bila kujua alijiingiza katika mapenzi na wanaume tofautitofauti mfano Bwana Ecko, Padre James, Salim, Kitunda na wengine.
Mwandishi anaona upo umuhimu wa jamii kueleweshwa vyema kuhusu mambo yanayopelekea kupatikana kwa ugonjwa huu hatari kama vile kuwa na mahusiano na wapenzi wengi. Mwandishi anapendekeza mambo ambayo anaona ni suluhisho la kuenea kwa ugonjwa huu zaidi. Mambo hayo ni pamoja na uwazi na ukweli katika hili, kutolewa kwa elimu juu ya Ukimwi, uadilifu, uaminifu katika ndoa, ngono salama, upendo kwa wagonjwa wa Ukimwi, msamaha na welewa. Hii ni kupitia barua ya Furaha aliyoiacha isomwe katika mazishi yake. Uk.44-45,
“Nawashukuru kwa kufika kwenu na kuyasikiliza maneno yangu ya mwisho. Msiogope kwani nadhani maneno haya yanaweza kuwasaidia.katika hii miezi ya mwisho nimelala kitandani nikifa,nikizidi kuugua. Nilipata muda mwingi wa kufikiri, kubadilika, kukua kama mtu; hata ninapokuwa ninakufa. Katika ukurasa unaofuata kuna orodha ya vitu ambavyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu, orodha ambayo inaonesha kwenu nyote ukweli juu ya kifo changu mama tafadhali wasomee watu wote orodha hii.”
Mmomonyoko wa maadili
Mmonyoko wa maaadili ni pale ambapo wanajamii huenda kinyume na makubaliano ya jamii yao, yaani taratibu, kanuni mila na desturi zao. Mwandishi anaona kuwa suala la mmonyoko wa maadili ni kichocheo cha maovu katika jamii. Anamtumia muhusika Mery na Furaha ambao ni vijana wadogo kabisa lakini wanajiingiza katika tabia zisizofaa kwani katika jamii yao waliwasema juu ya hili kwani walipotoka. Wazazi wa Furaha wanalipigia kelele suala hili lakini kijana wao tayari alishaharibika, mfano tunaona uk. 11 baba Furaha analaumu juu ya tabia ya Furaha anasema “ nilichokuwa nafahamu …. Hadi sasa Furaha… ni kwamba umekuwa ukitoroka nyumbani wakati wa usiku wa manane! Kuna jambo lingine ambalo anapaswa kulifahamu” anaendelea kusema “kutoroka… bila ruhusa… baa wanaume.. wewe …. Malaya usiye na shukrani!”.
Katika jamii ya leo wazazi wanapewa ujumbe kuwa suala la kuwaangalia watoto na kufuatilia nyendo zao ni jambo la msingi sana hasa katika kipindi kigumu cha makuzi. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kuikoka jamii toka katika hatari ya kupoteza vijana wengi zaidi.
Uaminifu katika ndoa na mahusiano
Mhusika Bwana Ecko hakuwa mwaminifu kwa mkewe kwani alikuwa malaya na aliyewaharibu mabinti wadogo waliokuwa kama wanae wa kuwazaa kiumri. Furaha anarubuniwa na kujikuta akitumbukia katika mapenzi na baba huyu. Mfano uk.6 tunaona Bwana Ecko anavosema“karibuni kwenye baa yangu. Karibuni kae nami, wapenzi!Bia mbili kwa ajili ya wasichana warembo”.Hali kadhalika katika kitabu Furaha anaelezwa kukosa uaminifu kwani licha ya kutembea na Bwana Ecko ila pia alijihusha na wanaume wengine kama Kitunda na Salim na hivyo kusababisha kuenea zaidi kwa ugonjwa huu.
Suala la upotofu wa uaminifu ni janaga katika jamii ya leo, kwani tunaona watu wazima sasa badala ya kuwa mstari wa mbele kuwasaidia mabinti wadogo kimaadili ila wao ndio wamekuwa mstari wa mbele katika kuharibu maisha yao. Ni tabia mbaya na inapaswa kupigwa vita.
Umaskini na hali ngumu ya maisha
Katika kitabu tunaona kuwa sababu mojawapo iliyopelekea Furaha kupata maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ni hali ya umaskini. Furaha alitamani vitu vizuri na hakujua madhara yake na namna ya kuvipata, alifurahia kuvipata na kujiona mwenye bahati. Mery anasemauk.7 -8 “nimekwambia hawa jamaa ni burudani…hata yule mshamba Juma. Sikia, pata burudani na kuwa mwema, kwa Ecko. Anaweza kukununulia vitu vingi sana! Unadhani wasichana wadogo hapa mjini wanapataje viatu vipya, magauni na mabegi mapya ili wapendeze….wapendeze kiasi cha kuwavutia vijana wazuri wa kiume?”
Mwandishi anaonesha hili kwani wasichana wengi hutumbukia katika janga la Ukimwi kutokana na umaskini. Anaona ipo haja ya watu kuelemishwa kuwa kila jambo lina wakati wake hasa kwa mabinti, washauriwe juu ya mambo mbadala ya kujipatia pesa na sio kujirahisisha kwa wanaume. Kumbe ni muhimu elimu ya ukimwi inapotolewa katika jamii basi pia watu hasa vijana waelekezwe pia namna ya kujikomboa kiuchumi, na waone kuwa ngono sio chanzo cha mapato bali wanapaswa kujibidisha ili kuwa na vipato vya kukidhi mahitaji yao ya muhimu.
Ukosefu wa uadilifu katika kazi
Padre James katika kitabu ameonekana kutokuwa muadilifu kuendana na maadili ya kanisa akiwa kama Padre. Anajisahau na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mtoto Furaha hali akijua kabisa ni kinyume na maadili na kazi yake ya upadre.Uk.10 “Furaha alikuja kama alivyoagizwa….ee.. Ekaristi takatifu ilipatikana lazima uelewe jinsi ilivyo vigumu kwa mtu wa hadhi yangu na wadhifa wangu”
Tofauti na ilivyotegemewa kuwa Padre James angekuwa mstari wa mbele kuiongoza jamii katika maadili mema. Lakini yeye ndiye anakuwa chanzo cha uharibifu wa maadili, suala hili lipo katika jamii kwani wapo watu ambao wameteuliwa kuwa kioo na taa ya jamii kumulika maovu lakini wao hutumia mwamvuli huo kujifunuika kufanya maovu kwa urahisi zaidi. Mwandishi ameona kuwa hili ni tatizo na anapingana kukemea vikali watu wa aina hii.
Umuhimu wa kusema ukweli na kuwa wazi
Hii ni suluhu mojawapo ambayo mwandishi anaamini kuwa ikitumika vyema basi ni kinga tosha dhidi ya Ukimwi. Baadhi ya watu hujielewa wazi kuwa tayari ni waathirika ila hawapendi kuwa wazi na kusema ukweli juu ya hilo, bali hunyamaza na kuendelea kuambukiza wengine. Mwandishi amemtumia mhusika Furaha na Mama Furaha kuwa mfano wa kuigwa kwani hawakuona haya juu ya kusema ukweli kuhusu ugonjwa uliomuua Furaha. Wanalisema hili mbele ya wanakijiji wote wakiwa na lengo la kuikomboa jamii yao.
Barua ya Furaha ni mfano toshauk.44-45. “kondom,uaminifu, elimu,welewa, uwazi,uadilifu, uwajibikaji, ukweli, upendo na msamaha,…ukosefu wa mambo yote haya ndio ulioniua. Ufuatiliaji wa mambo yote haya unaweza kuwaokoa ninyi nyote…wanusuruni watu wetu….wanusuruni watoto wetu ili wasiwe yatima. Muinusuru Afrika…yetu nzuri.”Pia hakumficha mchumba wake salim bali alimwambia ukweli uk.29 Furaha anasema“Nina Ukimwi Salim”
Suala la upendo
Upendo wa kweli ni ule ambao hujali kitu au mtu katika shida na raha, kujitolea kwa moyo wote bila kujali lolote. Ni kujitoa kwelikweli. Mwandishi analizungumzia jambo hili kama suala muhimu sana katika jamii. Tunapaswa kuonesha upendo kwa wagonjwa wa Ukimwi kwa kuwafariji na kuwapa matumaini, pia hata wahanga wa gonjwa hili kama vile watoto yatima ambao huachwa na wazazi wao wakiwa wadogo wanapaswa kupewa msaada na matunzo mazuri. Hawapaswi kunyanyapaliwa ila kupendwa.
Katika kitabu mhusika Mama Furaha ameonesha upendo wa kipekee kwa mwanae pamoja na hali aliyokuwa nayao Furaha jambo ambalo si rahisi kwa watu wengi. Mfanouk.30-31 Mama Furaha anaongea na mwanae akiwa hoi kitandani katika hali ya upendo na kujali anasema, “hakuna mtu aliye kamili. Lakini uliwaangalia wadogo zako. Na kila mahali ulipokuwapo, kulikuwa na nuru ya jua! Ulikuwa binti mzuri…binti yangu mzuri…. Inaelekea kama umezaliwa jana tu. Na hata wakati huo ulizidi kunifanya nisubiri, wakati nikiwa na mimba yako. Nakumbuka jinsi ulivyokua. Ukikmbia shambani mwetu, ukijaribu sana kumfurahisha baba yako…unajua anakujali kwa namna yake…..amelala sasa lala mwanangu”.
Imani potofu juu ya ukimwi
Wanakijiji katika kijiji cha Furaha wengi wao hawakuwa na elimu juu ya ugonjwa huu hatari, Furaha alipougua kila mmoja alisema lake wengine wakidai kuwa ni kurogwa. Pengine pia ujinga ulichangia wao kutoelewa kuhusu Ukimwi. Mfano uk.25-26 majibizano ya wanakijiji juu ya habari za kuumwa kwa Furaha.
Mwanakijiji wa 1: Bi Furaha anaumwa sana…
Mwanakijiji wa 2: Tulijua anaumwa
Mwanakijiji wa 1: Ndiyo lakini katibu katika ofisi ya daktari kanambia ana huu ugonjwa wa AIDS
Mwanakijiji wa 4: Hicho si kitu kizuri
Mwanakijiji wa 1: Wanauita slim kwa sababu ugonjwa wenyewe hukufanya ukondeane
Mwanakijiji wa 3: Lakini amewezaje kuupata ugonjwa kama huo!
Mwanakijiji wa 1: Rahisi! kuna mtu kamroga…. Pengine rafiki msichana mwenye wivu.
Mwanakijiji wa 2: Nasikia unaupata kwa kugusana tu!
Mwanakijiji wa 4: Au hata kuwa nao katika chumba kimoja!
Mazungumzo hayo yanatuweka wazi kuhusu haliiliyoko kijijini juu ya elimu kuhusu Ukimwi, wapo baadhi ya watu bado wanaamini kuwa Ukimwi ni kurogwa tu, serikali na mamlaka husika vinapaswa kutoa elimu ya kutosha katika jamii ili kuwakomboa watu walioko vijijini.
MIGOGORO
Mgogoro kati ya Furaha na wazazi wake: Sababu ya mgogoro huu ilitokana na Furaha kuanza kupotoka kimaadili. Kwani alitoroka nyumbani usiku na kwenda kwa wanaume baa kunywa pombe. Baba yake na mama yaake walimuadhibu kukemea suala hili.
Mgogoro kati ya Padre James na Mama Furaha: Sababu ya mgogoro huu ni orodha, Padre James alimzuia mama Furaha asisome barua yenye orodha kwani alihofia pengine jina lake lingetajwa miongoni mwa watu waliokuwa na mahusiano ya mapenzi na Furaha. Suluhisho la mgogoro huu Mama Furaha alimuweka wazi Padre juu ya umuhimu wa kuisoma barua hiyo kuwa hana la kuficha bali aliisoma kwa lazima uk.3 na 43.
Mgogoro kati ya Salim na Mama Furaha: Salim hakutaka orodha isomwe hivyo alichana barua yenye orodha mazishini. Mama Furaha hakusita bali aliisoma barua hiyo kwa kukusanya vipande na kuviunga. Uk.43 na 44.Mgogoro kati ya Furaha na Dada mdogo.Huu ulitokea pale ambapo Furaha alitaka kutoroka usiku na mdogo wake kubaini na hivyo kutishia kusema kwa wazazi. Suluhisho Furaha alimkemea na hata kutishia kumchinja uk.6 Mdogo wake aliogopa na kutosema lolote tena.
Mgogoro kati ya Slim na Furaha: Huu ulitokana na Salim kumlazimisha Furaha amsomee orodha yeye kwanza lakini Furaha aligoma na kumsihi asubiri. Ndipo Salim alipokasirika na kuanza kutupiana maneno. Mama Furaha anasuluhisha mgogoro huu kwa kumuamuru Salim atoke nje. Uk.30
Mgogoro wa nafsi: Huu uliwakuta Padre James, Salim, Kitunda, Bw Ecko baada ya kuhofia juu ya orodha ambayo Furaha aliiandika ili isomwe katika mazishi yake. Walihofia endapo wangetajwa katika orodha hiyo kwani wangeaibika mbele ya kijiji kutokana na kujua fika kuwa mambo waliyoyafanya ni kinyume na maadili. Wanajitahidi kuzuia orodha hiyo isisomwe kwa hali na mali, lakini hawafanikiwi. Mama Furaha anafanikiwa kusoma orodha hiyo na kutoa ujumbe kwa jamii nzima. Wanapata amani baada ya kujua kuwa orodha iliyosomwa haikuwa na majina yao.
FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa endapo jamii itaelimishwa juu ya ugonjwa wa Ukimwi ni rahisi kuepuka na kujikinga na maambukizi mapya. Hii ni kupitia mambo anayoyapendekeza mwandihi kama vile uwazi, uadilifu, ukweli, upendo, matumzi ya kondomu, elimu, welewa, msamaha, uaminifu.
MTAZAMO: Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu kwani anayaona mambo kwa udhati na uhalisia wake. Anapinga mtazamo wa kidhanifu juu ya ugonjwa wa Ukimwi kama vile kuamini kuwa ugonjwa huu unapatikana kwa kurogwa. Anaweka wazi sababu za upatikanaji wa ugonjwa huu.
MSIMAMO: Msimamo wa mwandishini wa kimapinduzi kwani analenga kuikomboa jamii kutoka katika hatari ya gonjwa la Ukimwi. Anapendekeza mambo ya kufanya ili kuepukagonjwa hili. Kama vile uaminifu, uadilifu, upendo, ukweli na uwazi nk.
UJUMBE
Elimu ya ukimwi ni muhimu kutolewa katika jamiiya leo.
Wagonjwa na wahanga wa Ukimwi wanapaswa kupendwa na kujaliwa.
Ukweli na uwazi ni suluhu mojawapo ya kuepusha maambukizi mapya.
Watu wazima wanaoharibu maisha ya watoto wadogo wanapawa kupigwa vita.
Upendo ni jambo la msingi kwa wahanga wa Ukimwi.Wazazi wanapaswa kuwa makini katikamalezi bora kwa vijana .Watu wanapaswa pia kukombolewa kiuchumi kama njia dhidi ya kupinga ukimwi.Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.Ulevi ni kichocheo cha maovu.

Maudhui katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliye
DHAMIRA
Umaskini na hali ngumu ya kimaisha:Watoto wa Mama Ntilie wanaishi katika hali ngumu sana kwani wanakosa shule sababu ya kukosa fedha, malazi, mavazi, chakula ni duni sana kwao. Tunaona kuwa hata kazi anazofanya Mama Ntilie ni kazi za vijungujiko kama anavyosema mwandishi uk.14, faida yake ni ndogo kwani haikidhi mahitaji ya familia. Mwandishi amejadili hili ili serikali na jamii kwa ujumla wake viweze kubuni mbinu za kuwakomboa akina mamawasiliano na ajira, wasio na kipato chochote au kipato cha chini sana. Ili kuepusha athari hasi za umaskini kama vile uhalifu, wimbi la watoto wa mitaani nk. Pia wakazi wengine wanalezwa kuwa na maisha magumu mfano uk.26 “watu walisongamana wakasukumana kugombania mchele ambao ….” Hii inatuonesha kuwa walikula vyakula vya jaani.
Jangala watoto wa mitaani:Katika kitabu hiki watoto Dan, Doto na Kurwa ni watoto wa mitaani. Hali hiyo imewakuta baada ya kukosa wazazi na malezi yao.. maisha yao ni ya shida mno yanayoenda kwa kudra za mwenyezi Mungu, kwani hula na kuvaa jalalani. Mfanao uk. 20,21-25-26. Suala hili ni janga sugu kwa nchi yetu kwani badala ya kupungua linaongezeka kwa kasi kwani watoto wa aina hii ni wengi mtaani na hawana dira yoyote ya maisha yajayo na kuwafanya kujiingiza katika shughuli zisizo halali ili kujipatia kipato.Suala hili limeoneshwa ili jamii na mamlaka husika viweze kuchuka hatua kwa kuwakomboa watoto hawa mfano kuwapatia elimu na mahitaji mengine ya msingi kwa watoto.
Suala la ukosefu wa elimu:Watoto wote wanaoelezwa katika riwaya hii kama Dan, Doto, Kurwa, Musa, Peter na Zitta hawana elimu na wala hawana ndoto za kusoma baadaye kutokana na hali halisi ya maisha yao. Wazazi wao hawamudu kuwapeleka shule, tunaona wanafukuzwa shule kutokana na kukosa sare za shule! Na ada!Uk.1 mwalimu Chikoya anasema “wote ambao hamna ada na hamna sare! hakunashule! nisizione sura zenu bila ada na sare waambieni hivyo wazazi wenu”.Suala la kuwafukuza watoto shule si jukumu lao bali la wazazi wao, kwani ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi. Jamii na serikali inapashwa juu ya hili ili watambue kuwa elimu kwa mtoto ni muhimu kwani ndio msinngi wa maisha yao. Na kuwasaidia wazazi wasio na uwezo wa kusomesha.
Uhalifu, wizi na ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya:Katika riwaya, watoto wadogo sana wameoneshwa kujiingiza katika sula la uhalifu mfano uuzaji wa madawa ya kulevya, wizi nk. Tunawaona vijana Dan na Doto wanajihusisha na wizi na hata kuhatarisha maisha yao na kufa. Uk.42-45. Kwa upande mwingine tunamuona mtoto Musa ambaye anajiingiza kwenye biashara haramu ya madawa ya kulevya. Anamshawishi pia Peter na kusababisha maisha yao kuishia jela.. mwandishi ameliangazia hili ili jamii iweze kuwa makini katika mienendo ya watoto kwa kuwalinda hasa kwa jamii ya sasa, ambapo vigogo huwatumia vijana wadogo katika biashara hii haramu. Wanatakiwa kuchukuliwa hatua na kuwajibishwa vikali.
Ulevi: Ulevi ni kikwazo cha maendeleo. Usemi huu unatokana na mambo aliyoyaonesha E. Mbogo katika riwaya kwani Mzee Lomolomo ni mlevi wa kupindukia na mwandishi anaeleza uk.10-13, juu ya Lomolomo ambaye hajui wanae wanaishije anachojua yeye ni pombe tu.Uk.49 “ratiba ya baba yao Mzee lomolomo………Ni mwanaume lofa kama asemavyo mwandishi kwani hajibidishi na kazi yoyote, naye anachangia ugumu wa maisha ya watoto wake. Suala la ulevi linahalisika katika jamii yetu ya leo katika familia zetu kwani baadhi ya wazazi huhusudu pombe na kusahausuala zimala malezi ikiwa ni wajibu wao! Wengi huishia kuharibu kazi, kuzua ugomvi, wizi nk. Mfano tunaona Mzee Lomolomo anakufa kutokana na tamaa ya pombe kwani anakunywa pombe ambazo zimepitwa na wakati na kumfanya afe.
Mapenzi: Katika riwaya mhusika Peter alionesha mapenzi ya dhati kwa Kurwa, kwani alimsaidia Kurwa uk.65 Peter anasema“tungoje mama arudi, lakini siwezi…. Hatuwezi kumfukuza, tukamwacha ateseke tu huko mtaani”.Pia tunaona mapenzi ya dhati ya Mama Ntilie kwa mumewe Mzee Lomolomo, kuwa pamoja natabia mbaya ya ulevi, kutofanya kazi na kutojali familia, kumsimanga na kumtukana lakini baado alimpenda na kumheshimu kama mumewe mfano alimpa chakula. Uk.13 pamoja na kuwa alilewa.
Nafasi ya mwanamke
Katika riwaya mwanamke amechorwa katika mtazamo tofautitofauti nzuri na mbaya:
Amechorwa kama mlezi na mhimiliwa familia. Mama ntilie ndiye aliyekuwa mlezi mkuu wa familia, bila yeye hakuna kilichowezekana katika familia, yeye ndiye aliyejua kula, kulala na kuvaa kwa wanawe. Wanawake wengi katika jamii huachiwa jukumu la kulea na wanaume kujisahau. Jamii imeoneshwa hili ili pande zote mbili zishiriki katika malezi.
Kama mtu mvumilivu: Mama ntilie ameoneshwa kuwa mvumilivu kwani alimvumilia mumewe pamoja na tabia yake mbaya. Anafundisha wanawake wengine kuwa wavumilivu kwani mvumiliivu hula mbivu!
Amechorwa kama muwajibikaji/ mchapakazi: Tofauti na wanawake wengine mama ntilie amekuwa machapakazi wa aina yake kwani pamoja na kipato kidogo alikuwa mfanyabiashara wa chakula katika kiwanda cha urafiki ambapo alipata pesa ndogo ya kujikimu yeye na wanae.Katika jamii ya leo wanawake wanaaswa kuwa wajasiriamali kwa kutafuta vyanzo vya riziki halali.
Amechorwa kama mtu mwenye huruma na roho nzuri: Mfano ni Jane ambaye alichukua jukumu la kuwalea watoto Kurwa na Doto ambao walifiwa na mama yao, kweli ni upendo wa kipekee. Pia Zenabu aliwahurumia Peter na Zita na ndiye aliyemsaidia Zita kwenda hospitali alipoumwa kichaa cha mbwa.
Amechorwa kama mtu mwenye wivu na roho mbaya: Mfano ni Zita, hii ni baada ya kuona Peter amemleta Kurwa nyumbani kwao. Hakuwa na upendo hata kidogo na hivyo kupigana naye kwa sababu ya chuki. Wanawake wanashauriwa kutokuwa na roho mbaya.
MIGOGORO
Riwaya ya watoto wa Mama Ntilie imejadili migogoro ya aina zote mbili ya nafsi na migogoro ya pande mbili.
Mgogoro kati ya Peter na Doto. Uk.20-22: Watoto hawa wawili walipigania masalia ya chakula jaani, Kurwa alisuluhisha ugomvi huo kwa kumzuia Doto kuendelea kumpiga Peter.
Mgogoro kati ya Mama ntilie na mzee lomolomo: Sababu ya mgogoro huu ni mzee lomolomo kuwa mlevi na kutoa matusi kwa mkewe aliporudi usiku.
Mgogoro kati ya Zita na Kurwa. Uk.60-64: Sababu ya mgogoro huu ni kuwa Zita hakumpenda Kurwa aje kwao mmoja wa familia yao. Walipigana hadharani, Peter alisuluhisha ugomvi huo kwa kumueleza Zita ukweli na kumkanya asimpige tena Kurwa.
Mgogoro kati ya zita na na Peter: Zita na Peter waliingia katika mgogoro baada ya Peter kufika nyumbani na Kurwa jambo ambalo halikumpendeza kabisa Zita. Peter alisuluhisha mgogorohuu kwa kumuambia hali halisi ya maisha ya Kurwa.
Mgogoro wa nafsia wa Kurwa: Kurwa aliwaza na kuihoji nafsi yake bila kuwa na majiu kuhusu ugumu wa maisha waliyokuwa nayo, kukosa wazazi hakuwa na jibu la mgogoro wake na hivyo kuendelea kujutia tu kuzaliwa. Uk.37-38.
Mgogoro wa nafsi kwa Peter: Aliwaza na kusumbuka ni lini angerudi shule kwani baada ya kufukuzwa na mkuu wa shule aliwaza ni vipi angepata pesa na wapi?, ili aweze kulipia karo na sare kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo huo.
FALSAFA: Imani ya mwandishi ni kuwa endapo watu watakombolewa na kufanya kazi kwa bidii wataukwepa umaskini na hali ngumu ya kimaisha. Mambo mengi anayoyaeleza anaishauri zaidi serikali kuwatazama wanawake kwa macho mawili na kuwasidia katika mitaji yao midogo.
MTAZAMO: Emmanuel Mbogo ana mtazamo wa kiyakinifu. Anayaona mambo kwa uhalisia wake ndani ya jamii. Anaona kwa umaskini na matatizo mengine ya kiuchumi na maisha hayatokei tu kwa kudra za mwenyezi Mungu bali ni mipango mibovu ya serikali, wananchi kutojishughulisha, malezi mabaya ya watoto.
MSIMAMO: Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani mambo anayoyaeleza ni kupiga vita kama vile umaskinina hali ngumu ya maisha, suala la ulevi, biashara ya madawa ya kulevya, wimbi la watoto wa mitaani. Haya ni mambo yanayotishia maendeleo ya jamii hivyo anasema makusudi ili jamii na mamlaka husika viweze kubadilika na kusaidia panapowezekana.
UJUMBE/MAFUNZO AU MAADILI
Tunafundishwa kuwa ulevi ni kikwazo cha maendeleo. Hivyo si budi kuupinga.
Suala la malezi ni jukumu la wazazi wote wawili na si la mama tu kama alivyofanya mzee Lomolomo.
Kuwafukuza watoto shule kwa ukosefu wa ada na sare ni makosa kwani ni kuwadidimiza watoto kielimu na kuwakosesha haki yao ya msingi.
Serikali na jamii vinaaswa kupunguza wimbi la watoto wa mitaani kwa kuwasaidia, si kuwaacha wateseke.
Uhalifu si mzuri kwani mwisho wake ni mbaya.
Tunafundishwa kuwa kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii ni suluhu ya maendeleo, tunamuona mama ntilie kupitia kazi yake ndogo aliweza kuikimu familia yake.
Umaskini na hali ngumu ya maisha ni tishio kwa jamii hivyo mwandishi anatuasa kufanya kazi kwa bidii ili kuushinda umaskini.
Upendo na huruma ni mambo mema na mazuri kwa jamii. Mfano Peter alimhurumia Kurwa na kumsaidia.
Wazazi wanaaswa kuwa makini katika malezi ya watoto na kutowaacha wajiamulie mambo. Mfano mzazi wa Musa alimuacha Musa na kupotea.
Uhakiki wa Maudhui katika Ushairi
Maudhui katika Ushairi wa Wasakatonge
DHAMIRA
Kupinga unyonyaji na ukandamizwaji.
Mashairi ya“Wasakatonge”, “Mvuja jasho”, “Sikuliwa sikuzama”, “Madikteta”ni mashairi yanayopinga na kukemea sula la unyonyaji na ukandamizwaji wa watu wanyonge wa tabaka la chini. Mwandishi amesema haya makusudi ili kukomesha mambo haya kwani huendelea kukuza utaaka katika jamii. Anaishauri serikali kuweka mikakati ya kuwakomboa wanyonge. Mfano katika shairi la“wasakatonge”anasema:

Pia katika shairi la“Mvuja jasho”mwandishi anawashauri wanyonge kushirikiana ili kujikomboa.
Kupigania haki na ukweli
Mwandishi pia anaona upo umuhimu wa jamii kutafuta na kuisimamia haki ya kweli. Anaona kuwa suala la haki likizingatiwa katika jamii itaepusha matatizo kama vile ya migogoro nk. Mfano wa mashairi ni shairi la“Kosa”, “Marufuku”.Mfano katika shairi la“Kosa”anasema:

Mwandishi ameonesha hali halisi ya baadhi ya wananchi walio wengi ambao kipato chao bado ni duni. Anaona sababu ya hali hii ni mifumo mibovu ya kiuchumi inayoendelea kukuza utabaka katika jamii kati ya walio nacho na wasio nacho mfano katika shairi la “Walalahoi”anasema:

Mashairi mengine ni“Waasakatonge”na“Mvuja jasho”
Kupiga vita matabaka katika jamii
Matabaka ni suala lisilo zuri katika jamii kwani husababisha walio chini kuendelea kukandamizwa na walio juu kiuchumi, kisiasa nk. Mfano wa mashairi yanayopinga ni “Miamba” na “Wasakatonge”. Mfano akatika shairi la “Miamba”

Umuhimu wa kutunza amani
Mwandishi analizungumzia suala la amani katika shairi la“Afrika”.Bado anaona jamii bila amani haiwezi kuendelea. Watu huhitaji amani ya kuishi pamoja na sio kwa vigezo vya ukabila au utaifa. Mfano anasema katika moja ya beti zake:

Suala la uongozi
Hapa uongozi umejadiliwa katika pande zote yaani uongozi mzuri na mbaya. Lakini mwandishi ana lengo moja la kuwafanya viongozi wasio waadilifu kubadilika na walio waadilifu kuacha. Anazungumzia kiongozi bora anatakiwa aweje anamfananisha na nahodha katika shairi la“Nahodha”anasema;

Mwandishi anafananisha nahodha wa ngalawa na nahodha wa nchi. Anaona kiongozi bora ni Yule anayeongoza kwa matakwa ya wananchi na sio matakwa yake binafsi. Anawataka viongozi walioshindwa kutawala waachie madraka kwa wenye uwezo huo. Pia yapo mashairi mengine kama vile“Madikteta”, “Saddam Hussein” ‘Unyama”ambayo yanakemea uongozi wa mabavu na unyonyaji. Haoni umuhimu wote kwaviongozi kutawala kwa mabavu bali watumie sheria na demokrasia ya kweli.
Vilevile anazungumzia viongozi walio wasaliti. Anaona kuwa viongozi wa aina hii ndio wanaokwamisha mendeleo. Walipewa madaraka lakini wanayatumia vibaya na kushindwa kutekeleza waliyoahidi. Mfano wa mashairi ni“asali lipotoja” na “waramba nyayo”
Ukombozi wa wanawake
Wanawake wakiwa ni watu muhimu sana katika jamii mwandishi anaona kuna umuhimu wa wao kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo. Anayasema haya katika mashairi ya “Wanawake wa Afrika”, “tohara”, “Mwanamke”, na “Mama ntliye”.Mfano katika shairi la“wanawake wa Afrika” anasema.

Pia mwandishi anapinga mila mila potofu kama vile tohara kwa wanawake katika shairi la“Tohara”.Kwani ina madhara makubwa kwa mwanamke kama vile kifo.
Suala la mapenzi na ndoa
Mwandishi amejadili kwa kiasi kikubwa kuhusu mapenzi ya kweli na ya dhati. Mfano katika mashairi ya “Nakusabiliya”, “Tutabakia wawili” “Nilinde” “Mahaba”.Mfano katika shairi la“mahaba”anasema;

Anakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;

Kupinga ukoloni mamboleo
Huu ni ukoloni ambao pamoja na nchi kupata uhuru wa kujitawala lakini bado huendelea kupitia njia zingine kuwakandamiza watu. Mwandishi anakemea hili na kuitaka serikali kuaangalia kwa makini suala hili.mfano katika shairi la“Wafadhiliwa” “Bundi”,na“Fahali la dunia”.Mfano katika shairi la “Wafadhiliwa”anasema;

Ukombozi wa kiuchumi
Suala la jamii nkukomboka katika masuala ya uchumi ni jambo la msingi sana. Mwandishi ankisemea hili katika shairi la“Klabu”

Maadili mema na maonyo
Maadili mema ndio msingi jkatika jamii. Mtu anapoenda kinyume na makubaliano ya jamii huyo huhesabiwa kuwa amepotoka kimaadili. Mwandishi amejadili mambo mbalimbali kuhimiza maadili mema na maonyo. Mfano ni;
Kupinga uovu:Katika shairi la “Kansa”, “Mtemea mate mbingu” anapinga suala la uovu nahimiza kutenda wema. Mfano katika shairi la“Mtemea mate mbingu”.
Kupinga mapenzi ya jinsia moja:Hili ni tatizo kubwa kwa jamii ya sasa. Kwani tamaduni ambazo si zetu zinavamia kwa kasi jamii ya leo. Mwandishi ameliona hili na kulisema katika jamii. Anaeleza matatizo ya kuwa na mapenzi ya jinsia moja katika shairi la“Jiwe si mchi.”
Tamaa sio nzuri:Mwandishi anakemea suala la tamaa. Anawashauri watu kuridhika na walivyojaliwa kwani tamaa mbele mauti nyuma. Anayasema haya katika shairi la “Si wewe?”
Umuhimu wa kujibidisha katika kazi:Ili upate mafanikio si budi kujibidisha tena kwa moyo wote. Mwandishi anasema kuwa vitu vizuri havipatikani bure tu. Bali mtu anapaswa kushughulika haswa. Mfano katika shairi la“Mcheza hawi kiwete”anafananisha bidii katika kazi na uchezaji wa ngoma.
Umuhimu wa kusoma na kuitumia vizuri elimu:Mwandishi pia anaona kuna umuhimu wa wanajamii kuwa na elimu kwani elimu ndio dira ya maisha. Si hivo tu anawaasa wanajamii kuitumia vizuri elimu pindi wanapoipata. Watoemchango chaya katika maendelo na maadili ya jamii badala ya kuchochea mmomonyoko wa maadili na kukwamisha uchumi. Amebainisha haya katika shairi la “Wasomi”;
FALSAFA: Mwandishi wa kitabu hiki anaamini kuwa matatizo katika jamii yanasababishwana watu wachache wanaonyonya watu wengine mfano katika masuala ya uchumi. Tabaka la wasakatonge linaendelea kukandamizwa na kuwa chini zaidi kwa sababu ya wachache tu. Anaamini ili jamii iweze kuwa na haki na usawa upo ulazima wa kufuta matabaka na kuboresha vipato vya watu wa chini. Aidha anaamini pia jamii ili iwe na amaendeleo na amani watu wanapaswa kuenenda katika maadili yaliyo mema.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi katika diwani hii ni wa kiyakinifu. Kwa sababu matatizo kama vile, hali ngumu ya kimaisha na kuwepo tabaka la walalahoi ni mifumo mibovu ya kiuchumi ikienda sambamba na matumizi mabaya ya pesa za umma, uzembe katika kazi, unyonyaji na unyanyasaji. Anatoa suluhisho linalowezekana katika jamii kwa kukemea yote yale yanayoenda kinyume na maadili sambamba na kuwawajibisha viongozi wasiotimiza wajibu wao. Anaona wanyonge wanaweza kukomboka kwa kuwa na ushirikiano nakusimamia ukweli popote pale.
MSIMAMO: Msimamo wa S. Khatib ni wa kimapinduzi. Analenga kupindua maovu, kupindua viongozi wasio waadilifu, anapindua mambo ambyo ni kinyume na maadili ya jamii zetu lakini pia anapinga suala la utabaka kataika jamii. Mambo hayo yanatufanya tuone kuwa kweli mwandishi analenga kuibadilisha jamii. Hajayafumbii macho maovu na dhuluma zinazoendelea katika jamii bali ameyaweka bayana ili watu wayafahamu na kujirekebisha.
UJUMBE
Kufanya kazi kwa bidii ndio msingi wa maendeleo.
Suala la utabaka katika jamii si zuri, hivyo si budi kulipiga vita.
Unyonyaji, ukandamizwaji na unynyasaji haufai kwani unadidimiza walio chini na kuwatweza wachache.Elimu ni ufunguo wa maisha.
Wasomi wanapaswa kutumia vizuri elimu walizopata.Haki na amani ni vitu muhimu hivyo si budi kuvidumisha.
Viongozi wasiowajibika wanapaswa kuachia madaraka na sio kung’ang’ania.
Mwanamke anatakiwa kukombolewa kutoka katika mila na desturi potofu.
Mataifa ya Afrika ili yaendelee yanapaswa kupiga vita ukabila.
Wanajamii wanapaswa kuwa waaminifu katika mapenzi na kuwa na mapenziya dhati.
Usaliti ni pigo katika mapenzi.

Maudhui katika Ushairi wa Malenga Wapya
DHAMIRA
Suala la uongozi bora na uwajibikaji
Suala la uongozi limejadiliwa katika pande zote mbili za uongozi mzuri na uongozi mbaya. Waandishi wameonesha yote haya wakiwa na lengo la kuikomboa jamii. Wamesisitiza kuhusu uongozi bora mfano katika shairi la “Payuka” anawaasa viongozi kuwa watekelezaji wa yale wanayoyaahidi na sio kuwa wapayukaji tu. Mfano ubeti wa pili anasema

Anakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;

Pia katika shairi la “Puuzo” anawakanya viongozi wasiowajibika kutekeleza majukumu yao na kuacha uzembe. Anawaasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani ni wajibu wao. Anasema katika ubeti wa kwanza

Ukombozi wa kiuchumi
Mwandishi anaona kuwa ili jamii ikomboke kiuchumi yapo mambo ya msingi kutekelezwa. Miongoni mwa mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu. Mfano katika shairi la “Charuka” tunaambiwa kuwa.

Pia anakazia suala la kilimo kama ndio msingi wa kujikomboa kichumi katika shairi la “Adui” na katika shairi la “Mkulima”anaonesha umuhimu wa kumthamini mkulima na kilimo. Vikiwa kama vigezo vya maendeleo nchini mwetu. Mfano katika shairi la “Adui” anasema;

Pia katika shairi la“Tuyazingatie haya”mwandishi anatajamambo ambayo anaamini kuwa yakizingatiwa yataweka uchumi kuwa imara kama vile, kuchapa kazi, kukomesha ubaguzi kutopora mali za serkali, kushirikiana, kukosoana na kuepuka tamaa. Mfano ubeti wa pili anasema;

Ukombozi wa mwanamke
Mwandishi kwa kutambua nafasi muhimu ya mwanamke katika jamii, hakusita kuikumbusha jamii juu ya kuwaheshimu, kuwathamini, kuwapa uhuru na kupinga tamaduni zote zinazomkandamiza mwanamke. Anaamini kuwa kumkandamiza mwanamke ni kuikandamiza jamii. Anayazungumzia haya katika shairi la “Kifungo”, “Hina inapapatuka”, “Raha”.Mfano katika shairi la“kifungo”ubeti wa saba anasema:

Suala la maadili mema na maonyo
Umuhimu Wa kuwa na kauli nzuri.Mwandishi katika shairi la “Ulimi” anawaasa watu kuwa ulimi mzuri kwa maana ya kuongea vizuri na watu kwa adabu, na heshima. Anaona kuwa ulimi ni kiungo kidogo lakini kinaweza kusababisha matatizo au mambo mazuri. Anauasa ulimi akisema;

Umuhimu wa kutenda wema kwa binadamu wenzetu:Mwandishi anaona kuwa wanajamii wanapaswa kutenda wema kwa wanajamii wenzao kwani matokeo ya wema ni mafanikio na shukrani. Anasema katika shairi la“Hisani hulipwa”

Umuhimu wa kuwa na subira katika maisha:Mwandishi anawaasa wanajamii kutokurupukia maisha hasa vijana. Katika shairi la “Siharakie maisha”Anaona upo umuhimu wa kufanya mambo kwa wakati na kuacha tamaa kwani kila jambo na wakati wake. Anawaasa wanafunzi kushikilia masomo na kutolimbukia mambo ambayo si wakati wake. Anasema;

Umuhimu wa kuishi vyema duniani:Katika shairi la “Ulimwengu”na“Maisha ni kama njia”mwandishi anaiambia jamii kuishi vizuri katika dunia kwani dunia ni mapito tu. Mfano katika shairi la“Maisha ni kama njia”anasema;

Uaminifu katika ndoa:Suala ndoa kwa jinsi anavyosema mwandishi uaminifu ndio jambo la msingi kwani huleta upendo na amani kwa familia. Anawashauri wanaume kujali familia zao na kuwa na mahusiano mengine nje ya ndoa. Katika shairi la“Kwanini”anasema;

Matumizi mazuri ya pesa:Mwandishi anaona upo umuhimu wa kutofuja pesa. Anashauri watu kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Anaona kuwa ufujaji pesa ni dhambi na si haki. Katika shairi la“Israfu”

Kuzingatia dini na kumuabudu Mungu:Mwandishi anawaasa wanadamu kutii maadili ya dini zao. Kwani misingi ya dini huelekeza watu katika mema. Anasema haya katika shairi la“Maisha ni kama njia”.Ubeti wa tano anasema;

Suala la Mapenzi:Katika shairi la “Ua” na katika shairi la “Nipate wapi mwingine”waandishi wanaona kuwa mapenzi ya dhati na ya kweli ni jambo jema. Anawataka watu kuthamini na kuwaheshimu wapenzi wao na binadamu wengine. Mfano katika shairi la“Ua”anasema;

Pia katika shairi la“Nipate wapi mwingine” mwandishi anazungumzia jinsi ilivyo kazi kupata mpenzi wa kweli. Dunia sasa imebadilika watu hupenda vitu vingine badala ya kuwa na mapenzi ya kweli yanayojali utu wa mtu. Mwandishi anayaita kuwa hayo ni mapenzi ya ulaghai. Mashairi ya“Utanikumbuka”linaasa juu ya usaliti katika mapenzi kuwa haufai. Shairi la “Kuunge” na“kitendawili”yanakazia zaidi juu ya kuwa na msimamo katika mapenzi.Anafananisha watu wasio na mapenzi ya kweli na Njiwa anayerukaruka asiyetulia. Mwandishi anasema;

Umuhimu wa wosia:Suala la kutoa wosia kwa mwanadamu ni jambo la muhimu sana pindi anapokufa. Suala hili huepusha migogoro na malumbano kwa wanafamilia wanaobaki. Katika shairi la “Niniwanangu” anasema:

Suala la ukombozi wa kifikra:Mwandishi anaitaka jamii kukomboka kifikra. Mambo haya anayazungumzia katika shairi la “Usiwebendera”. Suala la kuwa na msimamo binafsi na thabiti katika maamuzi ya mambo ni jambo la msingi katika maisha ya kila siku. Anaona kuna athari ya kuendeshwa au kuamuliwa mambo kama bendera inavofuata upepo.
Utetezi wa haki.Mashairi ya“Mpaka lini”, “Samaki mtungoni” “Sokomoko”yanazungumzia juu ya ukosefu wa haki. Mahali popote hapawezi kuwa na amani bila kuwepo haki. Hivyo mwandishi anaeleza;

Katika shairi la“Samaki mtungoni”mwandishi anaona kuwa kwa sababu ya ukosefu wa hik watu hudhulumiwa na kuteswa anafananisha wadhulumu haki na wavuvi anasema;

Utabaka na unyonyaji na unyanyaswaji:Mambo ya matabaka ndiyo yanayochangia kunyanyaswa, kunyonywa na kukandamizwa. Matabaka ambayo waandishi wanayazungumiza ni matabaka ya kiuchumi, kijamii na kisisasa. Katika shairi la“Samaki mtungoni”samaki anachorwa kama mtu mnyonge na mvuvi akiwa ni mwenye mabavu. Anaonesha jinsi watu wasivokuwa na uhuru bali kundamizwa na kuteswa. Hili limewekwa wazi ili kupiga vita mambo hayo katika jami. Anasema;

Vilevile katika shairi la“Punda” mwandishi anaelezea jinsi ambavyo watu wa hali ya chini wanavyoendelea kuonewa na kuteswa kama Punda. Anaishauri jamii kukemea suala hili na kusaidiana kuwainua wanyonge na sio kuendelea kuwanyonya.
FALSAFA
Falsafa ya waandishi wa mashairi ya “Malenga wapya” ni kuwa jamii inaweza kubadilika kiuchumi na kupata maendeleo kama itafanya kazi kwa bidii bila kuzembea, wanaamini kupingwa kwa utabaka na unyonyaji ni suluhu ya amani na maendeleo. Wanaamini pia ukiishi vizuri duniani utafanikiwa, wanasisitiza kutenda wema. Haki usawa na ushirikiano ni chachu ya maendeleo.
MTAZAMO
Mtazamo wa waandishi ni wa kiyakinifu kwani mambo wanayoyaeleza kama vile namna ya kutatua matatizo katika jamii. Mambo wanayoyapendekeza yanawezekana kutimizika mfano uwepo wa haki, kupinga utabaka, unyonyaji, kufanya kazi vizuri kuweka akiba na matumizi mazuri ya pesa na mambo mengine mengi.
MSIMAMO
Msimamo wa kimpinduzini msimamo wa waandishi wa diwani hii. Mambo wanayoyaeleza yanalenga kuleta mapinduzi katika jamii mfano kupiga vitu adui uvivu, kupinga dhuluma, kupinga maovu yote. Hiyo ni ishara kuwa wanalenga kuibadilisha jamii. Wanatoa pia changamoto na suluhu ya matatizo katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii kama vilekufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili.
UJUMBE
Kufanya kazi kwa bidii ni chachu ya mendeleo.
Uaminifu katika ndoa, mapenzi ya kweli ni jambo lamsingi.
Matumizi mazuri ya pesa husaidia kuwa na akiba nzuri na kupunguza umaskini usio na tija.
Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, si budi kukithamini.
Kauli nzuri huepusha migogoro na chuki.
Kumkomboa mwanamke ni kuikomboa jamii, hivo si budi kupinga tamaduni zinazomkandamiza.
Tunaaswa kupinga utabaka.
Kutetea haki na kupuuza unyonyaji ili kuleta usawa katika maisha.Viongozi walaghai na wasaliti hawafai kwa maendeleo hivyo tunaaswa kuwa makini kuchagua vingozi bora na kuwawajibisha wasiofaa.
Maudhui katika Diwani ya Chekacheka
DHAMIRA
Mwandishi amejadili dhamira mbalimbalizinazosawiri jamii yetu ya leo. Dhamira hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:
Uongozi bora
Suala la uongozi bora limejadiliwa na mwandishi wa diwani hii ikiwa kama jambo la msingi sana katika maendeleo ya Nchi. Mashairi ya“Mwinyi umewasha moto”na“indira”yanaelezea vyema juu ya viongozi ambao ni mfano wa kuigwa katika jamii.Mfano katika shairi la “Indira” anasema juu ya kiongozi Indira ambaye aliongoza vyema katika uongozi wake. Anawataka viongozi wa sasa kuiga mfano huo, anasema:

Pia hakuacha kugusia suala la viongozi wasiotimiza majukumu yao. Haya anayasema katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Utaliwa kama pumba” “Gunia la mikutano”mfano katika shairi la“Muwapi nawauliza”anawaamsha viongozi ili watimize majukumu yao:

Kupinga unyonyaji
Mwandishi anakemea masuala ya unyonyaji wa tabaka la chini. Shairi la“Kuna nini”, “Chatu mmeza matonge” “Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”.Mfano katika shairi la“Chatu mmeza matonge”mwandishi anazungumzia jinsi wanyonge wanavyoteseka katika hali ngumu ya maisha. Amelionesha hili ili jamii na serikali viweze kuwasaidia na kuwainua watu hawa.

Kupinga udikteta na ukosefu wa demokrasia
Suala la ukosefu wa demokrasia na haki ya kweli ni mambo ambayo yanafanya wanajamii kushindwa kujadili na kuweka wazi masuala nyeti ya kijamii pale inapobidi. Mwandishi kwa kuliona hili kama jambo la muhimu amelizungumzia katika mashairi ya“Raia si mali kitu”, “Dhahabu ya fahari”.

Kupinga ukoloni mamboleao
Mashairi ya“Lazima mniamini” na “Utumwa huru”ni mashairi ambayo yanaelezea juu ya ukoloni mamboleo. Mwandishi anaonesha kuwa nchi nyingi za kiafrika zimepata uhuru lakini ni uhuru wa maneno tu na si vitendo. Nchi hizi bado zinaamuliwa na kupangiwa mambo. Mwandishi anasema katika shairi la“Utumwa huru”anasema;

Ukombozi wa kiuchumi
Suala la ukombozi wa kiuchumi ni jambo ambalo huendana na maisha ya kila siku ya mwanadamu. Uchumi bora ndio huleta maendeleo zaidi katika jamii. Mwandishi analisema hili katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Kweli ilojaa udi”mfanokatika shairi la“Kweli ilojaa udi” anasemea juu ya uhaba wa bidhaa miaka ya themaninikwani uchumi ulizorota.

Kupiga vita matabaka
Shairila“Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”na“Gunia la mikutano”. Mfano katika shairi la “Gunia la mikutano”

Hapa mwandishi anajaribu kutuonesha utofauti kati ya wenye navyo au watawala na wasio nacho. Maisha yao ni tofauti kabisa. Wakati wengine wakifanya mambo ya anasa na starehe zisizo na tija wengine waumia kwa njaa na dhiki. Hivyo si budi jamii kwa pamoja kupinga suala hili kwa kuziba mifumo yote ya kitabaka.
Umuhimu wa Washairi kutunga mashairi bora
Bila kugusia masuala ya fani katika mashairi, Mashairi bora ni yale ambayo yanasema ukweli juu ya mambo jinsi ulivyo bila kificho. Ni mashairi yanayoangazia maisha ya kila mmoja katika jamii, hukosoa bila upendeleo wala hayasiti kusema na kutetea haki mara inapobidi. Shairi la“Tuambae ukasuku”ni shairi ambalo linawataka washairi kutunga mashairi wakiangalia matatizo ya jamii.
Suala la maadili mema na maonyo
Kuepuka tamaa: Katika shairi la “Moyo”mwandishi anauasa moyo kutokuwa na tamaa kwani unaweza kudhurika sababu ya tamaa.
Kuwa na uadilifu katika dini: Shairi la“Chanzo cha huo uozo”linaeleza juu ya aupotofu wa maadili kwa viongozi wa dini anawaasa kuzingatia misisngi ya imani zao na kuwa mfano katika jamii.
Kuthamini utu: Utu kuthaminiwa ni sehemu ya mambo muhimu sana kwa mwanadamu. Katika shairi la“Utu umekuwa kima”mwandishi naonesha jinsi ambavyo watu siku hizi hawatahmini utu na kuizingatia mambo mengine. Anaikumbusha jamii kuwa utu wa mtu ni muhimu sana kuthaminiwa.
Umuhimu wa kuwa na msimamo katika maisha: Shairi la“Chura umegundulika”linafananisha watu wasio na msimamo katika maisha na chura. Anawaasa watu kutokuwa kama chura kwa tabia yake ya kutoeleweka kama anaishi majini au nchi kavu.
Umuhimu wa kuwajali wazazi: Mwandishi kwa kutambua umuhimu mkkubwa wa wazazi, anaielimisha jamii kupitia shairi lake la“Ni wapi ushauri?”kuwa vijana wanapaswa kuwatunza na kuwasaidia wazazi wao pindi wanapozeeka.
Umuhimu wa kujiheshimu katika mapenzi: Shairi la “Penzi lisilo heshima”linakemea juu ya tabia mbaya ya watu wasiojiheshimu katika ndoa au mapenzi. Anakemea mapenzi ya pesa. Anashauri jamii kupendana kuthamini utu wa mtu na sio pesa.
Umuhimu wa kuwa na busara na hekima: Hekima ni jambo jema kwa mwanadamu. Mwandishi anaona kuwa kwa ktutumia hekima kuamua mambo ni vyema kuliko kukurupuka. Anayasema haya katika shairi la“Moyo”.
Kuepuka shari: Mwandishi katika shairi la“Moyo”anaiasa jamii kuepuka shari na ugomvi wala kutoichochea. Anawataka watu kuwa chanzo cha amani na mapatano.
FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa masuala ya haki na uwajibikaji ni suluhu ya maendeleo.
MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani kero na matatizo anayoyazungumzia katika jamii yapo kweli. Kama vile matabaka, uhujumu uchumi na hali ngumu ya maisha. Anatoa suluhu muafaka kwa matatizo hayo.
MSIMAMO: Msimamo ni wa kimapinduzi kwani mwandishi analenga katika kuibadilisha jamii. Anapinga masuala ya unyonyaji na ukandamizwaji. Pia anaona ipo haja ya viongozi na watawala kujituma kadiri inavowapasa. Mwandishi pia aligeuzia jicho masuala ya kimaadili kwani hakusita kuwakanya wavivu, waliopotoka katika uadilifu nk.
UJUMBE
Uadilifu katika dini na imani ni muhimu kuzingatiwa.
Haki na usawa ni suluhu ya migogoro ya kisiasa.
Wanajamii wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kukomboka kiuchumi.
Busara ba hekima ni mambo ya kuzingatia katika uamuzi wa jambo fulani.
Utu wa mtu unapaswa kuthaminiwa.
Washairi wanapaswa kuandika mashairi yanayoipasa jamii badala ya kuwa na ukasuku.
Mapenzi ya heshima na dhati ndio mapenzi ya kweli.
Matabaka katika jamii ni kikwazo na kichocheo cha unyonyaji hivyo si budi kupiga vita.